• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 7:50 AM
Jinsi ya kuandaa makange ya kuku

Jinsi ya kuandaa makange ya kuku

Na MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • kuku 1
  • mafuta lita 1
  • tangawizi iliyotwangwa vijiko vikubwa 3
  • kitunguu saumu kiliyotwangwa kijiko kikubwa 1
  • kitunguu maji 1
  • karoti kubwa 1
  • pilipili mboga 1
  • ndimu 2
  • chumvi
  • chicken masala vijiko 3
  • nyanya ya kopo kijiko 1
  • pilipili 1

Maelekezo

Osha kuku vizuri kisha kata mnofu uwe vipande kwa maumbo uyapendayo.

Weka kwa kuku viungo vyako kama tangawizi, kitunguu saumu, ndimu moja, na chicken masala vijiko viwili kisha changanya vizuri kabla ya kuweka kwenye jokofu kwa saa si chini ya mbili.

Kata karoti, pilipili mboga na kitunguu maji kwa urefu au umbo upendalo ila viwe vipande vikubwa vinavyoonekana baada ya kuiva.

Saga nyanya na iweke kwenye bakuli.

Chukua kikaangio, mimina mafuta hapo na yaache yapate moto wa wastani.

Anza kukaanga vipande vya kuku taratibu mpaka viive.

Tumia karai. Kwanza punguza mafuta ubakisha mafuta kiasi kwa ajili ya kukaanga viungo vilivyobakia.

Anza kukaanga kitunguu kisha weka pilipili mboga na malizia na karoti ila usikaange kwa muda mrefu kwa sababu havitakiwi kuiva sana.

Weka nyanya ulizosaga, koroga na malizia kwa kuweka chumvi, masala, nyanya ya kopo, pilipili na ile ndimu kipande kilichobakia.

Ingiza kwenye kikaangio vipande vya kuku na ukoroge kidogo ili navyo viungo vienee kisha epua na upakue kwenye sahani.

Chakula hiki kile pamoja na viazi, ndizi za kukaanga, ndizi za kuchoma, wali au chapati.

Angalizo

Hakikisha unapikia kwenye karai.

Usiweke maji wala nyanya nyingi wakati ukipika.

Rosti halitakiwi kuwa jingi; yatakuwa sio makange ni mchuzi sasa.

Kama huna kuku unaweza kupika kwa nyama ya ngo’mbe, mbuzi, samaki wa kukaanga na kadhalika.

  • Tags

You can share this post!

DINI: Neema itakufuata unapopanda mbegu maishani mwako na...

Raila yuko guu moja ndani Ikulu, Joho adai

T L