• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Jinsi ya kuoka mkate wa maboga, tangawizi na mdalasini

Jinsi ya kuoka mkate wa maboga, tangawizi na mdalasini

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 45

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • vikombe 2 unga wa ngano
  • kijiko 1 cha poda ya kuoka
  • kijiko 1 cha mdalasini
  • kijiko 1 cha iliki
  • kijiko 1 cha karafuu
  • kijiko ½ cha tangawizi
  • kikombe 1 cha puree ya malenge
  • kikombe 1 cha mtindi
  • vijiko 3 mafuta ya kupikia
  • vijiko 5 vilivyorundikwa vya sukari ya kahawia
  • mayai 3
Puree ya malenge. PICHA | MARGARET MAINA

 

Maelekezo

Anza kwa kutengeneza puree ya malenge. Hii inahusisha tu kumenya na kuchemsha malenge na mchakato huu utachukua kama dakika 10. Malenge yakisha kuwa laini kabisa, yaponde.

Utahitaji bakuli tatu kwa hatua zinazofuata. Katika bakuli la kwanza, changanya sukari ya kahawia na mayai mpaka yawe laini. Hakikisha unatumia sukari ya kahawia.

Katika bakuli lingine, changanya mafuta, puree ya malenge ambayo tumetayarisha tu na mtindi mpaka vyote viwe laini.

Katika bakuli la mwisho, changanya viungo kavu. Unga lazima upimwe kwa kutumia kikombe cha kupimia, si kikombe kingine chochote cha nasibu.

Mimina mchanganyiko wa sukari ya kahawia kwenye bakuli na viungo kavu, ikifuatiwa na mchanganyiko wa malenge na uchanganye vyote.

Kisha, mimina mchanganyiko wako kwenye chombo cha kuokea mkate kilichopakwa mafuta. Tunapaka mafuta ili mkate uweze kuondolewa kwa urahisi mara tu unapookeka.

Oka mkate wako kwenye ovena kwa nyuzijoto 170 kipimo cha Celcius kwa saa moja.

Epua na mkate uykishapoa, katakata na ufurahie.

  • Tags

You can share this post!

KINYUA KING’ORI: Wandani wa kinara wa Azimio...

Mabaki ya ndege yaopolewa ziwani

T L