• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 7:55 PM
Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwenye jokofu

Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwenye jokofu

Na MARGARET MAINA

[email protected]

HARUFU mbaya hutoka kwenye jokofu mara kwa mara.

Harufu inaweza kutokana na sababu tofauti. Kwa mfano, chakula kilichoharibika kikawa kimekaa sana bila kuondolewa kwa wakati.

Ili kuhakikisha kwamba jokofu ni safi, unapaswa kulisafisha mara kwa mara. Anza kwa kuondoa bidhaa zote, kisha ufute.

Kwa kuosha, unaweza kutumia dawa ya kuhifadhi harufu kwenye jokofu. Hizi kemikali za nyumbani za usafi, huondoa harufu mbaya kwa haraka tena kwa ufanisi mkubwa.

Utaratibu muhimu unaofaa ni huu:

Futa uchafu kwenye friji yako

Futa uchafu kwenye jokofu na lisafishe kabisa kwenye kuta na rafu.

Siki

Gawanya siki na changanya na maji kwa uwiano sawa. Itumie kufuta kuta zilizosafishwa. Vile vile safisha rafu. Acha kwa muda mlango wa jokofu ukiwa wazi ili harufu ya siki itoweke.

  • Kusafisha kuta zote za ndani kwa kutumia sabuni ya vyombo; dishwashing.
  • Kuifuta kwa mchanganyiko wa maji na limau.
  • Tumia adsorbent – itapunguza asilimia ya uchafu ndani ya chumba na kuondoa harufu ya ukungu.
  • Kutupa vyakula vyote vibaya.

You can share this post!

Poland na Uingereza nguvu sawa katika mechi ya kufuzu kwa...

Lempurkel akana shtaka la kueneza chuki Laikipia