• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 7:02 PM
Kiswahili na Viswahili: Je, kuna haja au hatari yoyote ya kuwa na aina moja tu ya Kiswahili Sanifu?

Kiswahili na Viswahili: Je, kuna haja au hatari yoyote ya kuwa na aina moja tu ya Kiswahili Sanifu?

NA PROF IRIBE MWANGI

MNAMO Novemba 24 mwaka jana (2022), niliandika kumhusu Mzee Abdilatif Abdala nikasema: (yeye ni) jagina, ustadh, gogo, gwiji na Profesa wa Kiswahili.

Mara ya mwanzo “nilipokutana” naye … ilikuwa kwa hisani ya Profesa Kineene aliponitanguliza kwa Sauti ya Dhiki.

Nilipoyasoma mashairi yake, nilipata taswira ya mtu mkali, mwenye vurugu na fujo.

Taswira hii iliyeyuka nilipokutana naye mara ya kwanza nchini Ujerumani mnamo 2016. Nilishtukia kuwa ni muungwana, mpole, mcheshi na maridhia.

Hata hivyo, leo naona nilikosea kidogo. Mzee Abdilatif kwa hakika husababisha vurugu, lakini vurugu nzuri, vurugu ya kiakili!

Maneno aliyoyatamka juzi katika Chuo Kikuu cha Zanzibar yamewavuruga akili wasomi wa Kiswahili kwelikweli!

Abdilatif alionya kuwa tukishikilia kuwe na aina moja tu ya Kiswahili Sanifu, tutakuwa tunahatarisha hali na maenezi ya Kiswahili.

Mjadala umekuwa, je, kuna haja ya kuwa na aina moja tu ya Kiswahili Sanifu?

Kuna wale wanaosema kuwa ni muhimu sana na kwamba ndio sababu kukawa na usanifishaji mnamo 1930. Wengine wamesema si muhimu na kuwa hata lugha nyingine kama Kiingereza zina “visanifu” vingi.

Baadhi wanasema kuwa tayari Kiswahili Sanifu si kimoja. Wanatoa mifano ya matumizi ya maneno kama ‘uzamili’, ‘uzamifu’, ‘matatu’, ‘onyesha’ na ‘mshipi’ nchini Kenya na ‘umahiri’, ‘uzamivu’, ‘daladala’, ‘onesha’ na ‘mkanda’ nchini Tanzania kwa maana ileile. Wazanzibari huzungumza kuhusu ‘kamusi la’ na ‘gari imefika’ ilhali Bara wanatumia ‘kamusi ya’ na ‘gari limefika’.

Je, hali hii inaonyesha kuwa kuna Viswahili Sanifu vya kimaeneo?

  • Tags

You can share this post!

NDIVYO SIVYO: Tofauti iliyopo baina ya maneno ‘moyo’ na...

Majangili waua wengi licha ya onyo la waziri

T L