• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 10:55 AM
Kongamano kujadili mifumo ya afya barani laanza

Kongamano kujadili mifumo ya afya barani laanza

NA PAULINE ONGAJI akiwa KIGALI, Rwanda

KONGAMANO la Kimataifa kuhusu Afya ya Umma barani (CPHIA 2021) liling’oa nanga Jumanne jijini Kigali, Rwanda, dhamira ya makala hayo ya pili ikiwa ni kuangazia mifumo ya afya barani.

Akizindua rasmi kongamano hilo, Waziri Mkuu wa Rwanda, Bw Edouard Ngirente, alisema kwamba kwa mataifa ya Afrika kutimiza ndoto ya afya kwa wote, sharti mifumo ya afya iwe thabiti.

Kupitia ujumbe wake mtandaoni, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la afya Duniani, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisisitiza haja ya kuthibitisha mifumo ya afya kama njia ya kujiandaa kukabili majanga yajayo ya kiafya.

Hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa kuhusu Afya ya Umma barani (CPHIA 2021) lililong’oa nanga Jumanne, Desemba 13, 2022 jijini Kigali, Rwanda, dhamira ya makala hayo ya pili ikiwa ni kuangazia mifumo ya afya barani. PICHA | PAULINE ONGAJI

Akiwasilisha maono ya kuhakikisha mifumo thabiti ya kiafya barani, kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia maradhi barani Afrika (Africa CDC), Dkt Ahmed Ouma, alisema wakati umewadia kwa nchi za Afrika kuwekeza katika mifumo thabiti ya kiafya.

Mwenyekiti mshirikishi wa CPHIA 2022 Profesa Senait Fisseha, alisema wakati umewadia kwa Afrika kuchukua nafasi yake katika jukwaa la afya kimataifa.

Kongamano hilo liliandaliwa na Muungano wa Afrika (AU), Africa CDC), CPHIA kwa ushirikiano na Wizara ya Afya ya Rwanda, na linatarajiwa kukamilika hapo Alhamisi Desemba 15.

  • Tags

You can share this post!

Profesa Oduor: Mifumo ya Bioteknolojia hupitia kaguzi za...

Mabaki ya watu waliozikwa miaka 5,000 yapatikana Ziwa...

T L