• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
LISHE: Fahamu faida za kula nyanya mbichi zilizoiva vizuri

LISHE: Fahamu faida za kula nyanya mbichi zilizoiva vizuri

NA MARGARET MAINA

[email protected]

NYANYA ni chanzo kikuu cha lycopene, ambayo imehusishwa na faida nyingi za kiafya, pamoja na kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na saratani.

Pia ni chanzo kikubwa cha vitamini C, potasiamu, folati, na vitamini K.

Nyanya ni nzuri kwa ngozi yako

Nyanya zina kiwango cha juu cha lycopene. Menya nyanya kisha paka kwenye uso. Acha nyanya kwenye uso wako kwa angalau dakika kumi, kisha osha. Uso wako utabaki ukiwa safi na unaong’aa.

Nyanya husaidia kudumisha mifupa yenye nguvu

Nyanya zina kiasi kikubwa cha kalsiamu na Vitamini K. Virutubisho hivi vyote viwili ni muhimu katika kuimarisha na kufanya marekebisho madogo kwenye mifupa pamoja na tishu za mifupa.

Damu safi yenye afya

Nyanya zina kiasi kikubwa cha Vitamin A na Vitamin C. Hii ni hasa kwa sababu vitamini hizi na beta-carotene hufanya kazi muhimu kwenye damu. Kumbuka, kadiri nyanya unayokula inavyokuwa nyekundu, ndivyo inavyokuwa na beta-carotene zaidi. Kupika nyanya huharibu Vitamini C, hivyo kwa faida hizi, ni vyema kula nyanya zikiwa mbichi.

Nyanya ni nzuri kwa moyo wako

Kwa sababu ya vitamini B na potasiamu katika nyanya, zina ufanisi katika kupunguza viwango vya lehemu na kupunguza shinikizo la damu. Kwa hivyo, kwa kujumuisha nyanya katika lishe yako ya kawaida, unaweza kuzuia shambulio la moyo, kiharusi na shida nyingine nyingi zinazohusiana na moyo ambazo zinaweza kutishia maisha yako.

Nyanya ni nzuri kwa nywele zako

Vitamini A katika nyanya hufanya kazi kikamilifu ili kuweka nywele zako zing’ae na zionekane zenye nguvu. Pia husaidia macho yako, ngozi, mifupa na meno.

Nyanya ni nzuri kwa figo zako

Kuongeza nyanya bila mbegu kwenye lishe yako husaidia kupunguza hatari ya mawe kwenye figo.

Nyanya ni nzuri kwa macho yako

Vitamini A inayopatikana kwenye nyanya ni nzuri kwa kuboresha nuru ya macho. Aidha, kula nyanya ni mojawapo ya vyakula bora vya kula ili kuzuia maendeleo ya upofu wa usiku. Nyanya zimejaa madini aina ya chromium. Inafanya kazi kwa ufanisi kusaidia wagonjwa wa kisukari kuweka viwango vyao vya sukari kwenye damu chini ya udhibiti bora.

  • Tags

You can share this post!

UJASIRIAMALI: Watumia teknolojia kupata wateja wa mboga na...

Mswisi na mpenziwe washtakiwa kwa kutolipa gesti Sh234,000

T L