• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
KAULI YA MATUNDURA: Baadhi ya tamathali za usemi ambazo ndilo shina la uhai wa lugha

KAULI YA MATUNDURA: Baadhi ya tamathali za usemi ambazo ndilo shina la uhai wa lugha

Na BITUGI MATUNDURA

JUMA lililopita, nilidai kwamba matumizi ya tamathali ya usemi huipa uhai insha au kazi yoyote ya kisanaa.

Nilitalii tamathali chache za lugha ya Kiswahili ikiwemo tasfida na tashibiha au tashbihi.

Tofauti kati ya tashbiha na sitiari ni kwamba, sitiari haitumii maneno ya viungo kama hayo ambayo tumeyataja kwenye tashbiha. Ulinganisho katika sitiari hufanya kitu kimoja kisemwe kuwa ni kingine. Kwa mfano: Nywele za Agnita ni kichaka, au maisha ni moshi, wakati titi la nyati – hukamuliwa kwa shaka na kadhalika.

Tashihisi nayo ni tamathali ambapo vitu visivyokuwa na uhai hupewa uhai. Kwa mfano: Miale ya jua la asubuhi yenye rangi ya kikahawia ilibusu vilima ambavyo viliishangilia kwa nyimbo zenye makeke.

Tasfida nayo ni tamathali ya usemi ambapo makali ya jambo fulani hupunguzwa kwa sababu ya kudumisha adabu katika mazungumzo au maandishi. Kwa mfano, si adabu kusema moja kwa moja kwamba: Juma amekwenda kunya. Ili kupunguza makali ya kauli hii ambayo kwa vyovyote vile inavunja kaida za adabu, watu husema: Juma amekwenda kuchepuka, au kutema mate au amekwenda kujisaidia au amekwenda pembeni au msalani.

Aidha watu husema, mwanamke amejifungua wala si kuzaa au mtu ana mkono mrefu badala ya mtu ni mwizi.

Takriri au msisitizo ni tamathali itumiwayo kutilia mkazo jambo. Katika riwaya ya Euphrase Kezilahabi, Rosa Mistika, tunaelezwa jinsi jamaa za Zakaria walivyorithi mali yake: Hawa jamaa walirithi. Walirithi hawa jamaa. Walirithi, walirithi.

You can share this post!

GWIJI WA WIKI: Geoffrey Mwamburi

Mtiririko wa vitushi, wahusika na maudhui Sura ya 7 –...

T L