• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Mtiririko wa vitushi, wahusika na maudhui Sura ya 7 – Chozi la Heri

Mtiririko wa vitushi, wahusika na maudhui Sura ya 7 – Chozi la Heri

Na JOYCE NEKESA

Juma lililopita tuliangazia hali geni aliyokabiliana nayo Umu na jinsi wanafunzi wenzake (Kairu, Mwanaheri na Zohali) walivyomshauri kuzingatia masomo yake kupitia kwa masimulizi na masaibu yaliyowakumba.

Leo hii tutaangazia masaibu yaliyomkumba Chandachema kupitia masimulizi yake.

Mtiririko wa vitushi

Alilelewa na nyanyake aliyeaga dunia akiwa katika darasa la kwanza. Babake alihamia ughaibuni pamoja na aila yake. Chandachema aliishi kwa Satua kwa muda mfupi baada ya mauko ya nyanyake. Satua alikuwa jirani yao na alikuwa na watoto watatu. Chandachema aliambiwa kuwa mamake, Rehema, alitoka Pwani alikokutana na Fumba (babake Chandachema) aliyekuwa mwalimu wake Rehema akiwa katika kidato cha tatu. Rehema na Fumba walikuwa na uhusiano wa kimapenzi ambao matokeo yake ni Chandachema aliyepelekewa nyanyake kumlea baada ya wazazi wa Rehema kukataa kumuoza binti yao kwa aliyekuwa mwalimu wake.

Chandachema alitoroka kwa Satua(Jirani) baada ya kuhisi mabadiliko ya kukataliwa na mhisani wake na kuenda katika Shirika la Chai la Tengenea kutafuta shule au ajira huko.Alienda katika Shule ya Msingi ya Kilimo alikomsimulia mwalimu mkuu,Bi Tamasha,masaibu yake.Alipewa nafasi katika darasa la pili.Alimkabidhi Chandachema Bw Tenge na mkewe Kimai ili wampe makao.Aliishi na familia hii pamoja na watoto wao watano katika mtaa wa mabanda.Walilala karibu na mvungu wa kitanda cha wazazi wao na kusikia kila lililotukia kitandani.Bwana Tenge aliwaleta wanawake wengine mkewe aliposafiri.Alipofika darasa la tano,Chandachema alijitafutia riziki kwa kuchuma majani chai.Alifanya mtihani wa darasa la nane na kufaulu.Alipewa makao na shirika la Kidini la Hakikisho la Haki na Utulivu lililowafadhili na kuwapa makao watoto mayatima.Chandachema ana ndoto ya kuwa mwanasheria ili atetee haki za watoto.

Maudhui

Maudhui yanayojitokeza katika sura hii ni ainati mathalan: Elimu imeangaziwa kama mojawapo ya haki ya kimsingi ya mtoto,shule ya Tangamano inatekeleza jukumu hili.Dhuluma/Ukatili/Ukandamizaji-wafanyakazi kwenye mashamba ya michai wanadhulumiwa na waajiri wao wanaowahamisha kila uchao bila kuzingatia kwamba wana watoto wanaopaswa kusoma katika shule moja (uk 107),Zohali anaachiwa kazi zote za nyumbani anapoambulia ujauzito.Babake anakataa kumlipia karo ya shule (uk 101),Fumba alimdhulumu kimapenzi mwanafunzi wake Rehema na kumringa akiwa katika kidato cha tatu(uk 103)

Haki za watoto zimeangaziwa pale ambapo watoto wanahiniwa haki zao.Haki za malezi na elimu za Kairu, Mwanaheri, Zohali na Chandachema zinakiukwa.Ukarimu unajitokeza pale Julida anapomkaribisha Umulkheri na kumhakikishia usalama hadi akabidhiwe Idara ya Watoto(Uk89), Marafiki wa Umu shuleni wanamhimiza kwa ukarimu avumilie maisha ya shule mpya.Mtawa Pacha anamwonyesha Zohali ukarimu kwa kumuokoa kutoka njia ya uharibifu(Uk99),Bi Tamasha, mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi ya Kilimo alimsaidia Chandachema (uk105), Baada ya kutengana na aila ya Bw na Bi. Tenge, Chandachema aliokolewa na Shirika la Hakikisho la Haki na Utulivu.

Usaliti-wazazi wa Zohali wanamsaliti walipomtelekeza baada ya kupata mimba.Maudhui ya Matumaini – Umu anajipa tumaini la kuanzisha na kuyazoea maisha ya jijini( uk85),Mwanaheri ana matumaini ya kuyaboresha maisha yake kwa kujikita katika elimu ili afanikiwe maishani,Chandachema anajipa tumaini la kufaulu maishani anapoazimia kutumia kipawa chake masomoni kuulainisha mustakabali wake(uk104).

Malezi yanajitokeza kupitia kwa Zohali na Chandachema,mimba za mapema kupitia kwa Zohali na Rehema.

Joyce Nekesa

Shule ya Kitaifa ya Kapsabet Boys

You can share this post!

KAULI YA MATUNDURA: Baadhi ya tamathali za usemi ambazo...

Inshallah nchi yetu iwe na amani zaidi mwaka 2022

T L