• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
KAULI YA MATUNDURA: Jinsi ya kumtambua mwandishi chipukizi wa tungo za kibunifu

KAULI YA MATUNDURA: Jinsi ya kumtambua mwandishi chipukizi wa tungo za kibunifu

Na BITUGI MATUNDURA

HATUA ya kutangazwa kwa orodha fupi ya wanaowania tuzo ya Mabati-Cornell Kiswahili Prize for African Literature – makala ya 2021 ilizua mdahalo miongoni mwa wataalamu na waandishi wa kubuni nchini Kenya.

Mjadala huo ulitokana na orodha hiyo kuwa na majina ya waandishi wa Tanzania pekee, bila hata mmoja kutoka Kenya.

“Wakenya hawaandiki? Au hawakushiriki kwenye kinyang’anyiro hiki?” Nikauliza wataalamu wa Kiswahili katika ukumbi mmoja wa kundi la WhatsApp.

Mwalimu Alex Ngure alinijibu kuwa swali hili lilikuwa limeibuka katika kundi jingine tofauti na kujibiwa na Dkt Salma Omar Hamad, mmoja wa wanajopo la uamuzi.

Mhakiki, Prof Mwenda Mbatiah aliongeza kuwa, katika ukumbi tofauti pia alisikia jawabu la kushangaza kuhusu swali lilo hilo: “Tuzo ni ya waandishi chipukizi – ili kuwakuza. Kwa hiyo, waandishi waliobobea wasipoteze muda wao kushiriki kwenye shindano hilo.”

Nilimjibu Mwalimu Mbatiah: “Hapo ndipo tunakwenda tenge. Je, ikiwa tuzo hii ni ya waandishi chipukizi, inaonekana Kenya haina waandishi chipukizi. Ikiwa wapo, ama hawaandiki, au ikiwa wanaandika, basi ni waandishi wa masafa mafupi.”

Dhana ya chipukizi huzua fahiwa ya kuwa ndio kwanza waandishi wanaingia katika utunzi. Ubobevu huzua fahiwa ya wale walioandika na kufahamika labda kutokana na ubora wa tungo zao, na pengine wingi wake.

You can share this post!

UCHAMBUZI WA FASIHI: Ploti ya Onyesho la Kwanza Tendo la...

NDIVYO SIVYO: Sahihi ni ‘Hamjambo’ wala si...

T L