• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Utangulizi wa uchambuzi wa hadithi ‘Tulipokutana Tena’

Utangulizi wa uchambuzi wa hadithi ‘Tulipokutana Tena’

Na GRACE OGOYE

IFUATAYO ni sehemu ya utangulizi inayochambua hadithi ya ‘Tulipokutana Tena’ yake Alifa Chokocho katika Diwani Tumbo Lisiloshiba.

a) Wahusika

i) Sebu na Tunu

ii) Kazu na Temu

iii) Bogoa na Sakina

iv) Bi. Sinai na wanawe

v) Wazazi na nduguze Bogoa

b) Mandhari

i) Club Pogopogo

ii) Kijijini

c) Mtiririko

Sebu, Kaze na wake zao wanajumuika ‘Hotel Rombeko’.

Wanataniana kuhusu imani za kishirikina zinazohusishwa na jamii tofauti. Maongezi yao yanamgusia Bogoa Bakari, ambaye ni sadfa wote wanamfahamu.

Sebu alimjua alipolelewa na jirani yake kijijini Zewa. Kazu naye anamfahamu alipofika jijini Seka kujitafutia maisha.

Wana hamu ya kukutana naye baada ya muda mrefu. Wanapanga kukutana ‘Club Pogopogo’. Bogoa anawapasulia mbarika kuhusu aliyoyapitia mikononi mwa Bi. Sinai na kutoweka kwake. Wanafurahia kukutana tena.

d) Dhamira

Mwandishi anakashifu wazazi wanaotelekeza jukumu lao la ulezi wa wana na kuwaachia walezi wa kupanga wanaowadhulumu wana hawa. Hisia za watoto husika hupuuziliwa mbali, na kusababisha utengano wa familia.

c) Maudhui

i) Umaskini huwasukuma wazazi kuwatelekeza wana wao. Wazazi wake Bogoa waliona nafuu kupunguziwa midomo ya kulisha ndiposa wakampeleka kwa Bi. Sinai.

ii) Malezi ya wana ni jukumu la msingi la wazazi, ndio wanaweza kuwapa wana mapenzi . Bogoa alipokuwa nyumbani, alikosa mahitaji lakini mapenzi yao wazazi yalifidia upungufu huu. Bi. Sinai naye, aliahidi kumlea Bogoa, lakini alimgeuza kuwa kijakazi wake.

iii) Unafiki unajitokeza kumpitia Bi. Sinai ambaye hakumpeleka Bogoa skuli wala kumpa nafasi kumwelezea wazazi wake ukweli walipowatembelea kule mjini. Alifanya kazi za nyumbani wenzake wakienda kusoma.

iv) Urafiki wa kweli hudumu. Sebu na Bogoa walikuwa marafiki wa chanda na pete utotoni. Ni watu wazima na bado wana hisia za kidugu, hisia zinazomsukuma Sebu kumtafuta baada ya miaka mingi. Wanacheza kwa furaha na kusherehekea kukutana tena.

v) Elimu ni ufunguo wa maisha. Sebu, Kazu na wake zao wameelimika na wanajiweza maishani. Elimu yao imewawezesha kufurahia maisha. Wanaweza kuzuru sehemu tofauti kujipumzisha.

vi) Bogoa analipiza kisasi kwa wazazi wake kwa kujitenga nao milele. Anawalaumu kwa maisha magumu anayoyapitia mikononi mwa Bi. Sinai. Anapotoroka, harejei nyumbani, anakosa hata kuhudhuria mazishi yao.

vii) Watoto wa kulelewa hufanyiwa ubaguzi. Bogoa hakuruhusiwa kucheza na wanawe Bi. Sinai. Alikula baada ya kila mtu, makombo kwenye sufuria na vyungu wenzake wakila sahanini. Wenzake walipoenda shule, alibakia nyumbani kufanya kazi na kupika mandazi ya kuuza.

Uchambuzi huu utaendelea wiki ijayo.

Grace Ogoye

Kisumu Girls High School

  • Tags

You can share this post!

KINYUA BIN KING’ORI: NCIC ikomeshe wanasiasa ambao...

Mlima Kenya kuwa na wagombea urais wawili Kabogo akijiondoa

T L