• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kupika magimbi ‘nduma’

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kupika magimbi ‘nduma’

NA MARGARET MAINA

[email protected]

MAGIMBI au ‘nduma’ ni mizizi ambayo ni chanzo kizuri cha wanga.

Magimbi huwa na kalori chache yana virutubisho vya kiwango cha juu na pia ni chanzo kizuri cha madini ya chuma na shaba.

Magimbi huwa na kalori chache sana ukilinganisha na vyakula vingine vya wanga kama viazi vikuu, viazi au mihogo.

Nyuzinyuzi kwenye ‘nduma’ ni muhimu na husaidia mfumo wa kusaga chakula kwani husaidia kusogeza chakula kupitia matumbo kwa njia bora, huku pia zikichochea uchukuaji wa virutubisho. Magimbi husaidia katika kupunguza athari ya sukari kwenye damu.

Muda wa kuandaa: Dakika 5

Muda wa mapishi: Dadika 20

Walaji: 3

Vinavyohitajika

  • Magimbi 4
  • Maji lita 2
  • Chumvi

Maelekezo

Osha magimbi ukishakwangua ngozi ya juu kisha kata upate vipande vidogovidogo.

Bandika sufuria yenye maji kwenye meko huku moto ukiwa ni wa wastani.

Weka magimbi na uyafunike yaanze kuchemka polepole kwa dakika 20.

Yakiiva epua, yaache yapoe.

Pakua na ufuahie kwa chai au nyama.

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa mchuzi wa kuku

MAPISHI KIKWETU: Jinsi ya kuandaa wali wa...

T L