• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 7:15 PM
MAPISHI KIKWETU: Saladi ya kuku, maembe na tango

MAPISHI KIKWETU: Saladi ya kuku, maembe na tango

NA MARGARET MAINA

[email protected]

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 20

Walaji: 2

Vinavyohitajika

  • maembe 2 uyakate kwa maumbo ya mchemraba
  • tango lililokatwa kwa vipande vya mchemraba
  • gramu 50 za mahindi matamu
  • kikombe 1 cha zabibu
  • nyanya 1 iliyokatwa

Kwa kuku

  • gramu 500 za kipande cha kuku bila mifupa
  • kijiko 1 cha sosi ya Soya
  • vijiko 5 vya siki ya Balsamu
  • kijiko 1 cha poda ya vitunguu (au karafuu punje 3)
  • kijiko ½ cha binzari nyembamba
  • vijiko 3 vya zaatari yaani thyme

Kwa juu

  • kikombe ½ cha mafuta ya alizeti
  • pilipili
  • binzari nyembamba
  • kijiko 1 cha tangawizi iliyosagwa
  • kijiko 1 cha asali
  • juisi ya limau
  • majani ya giligilani

Maelekezo

Ongeza viungo vyote kwenye bakuli na uvichanganye vyote pamoja.

Mahindi matamu na tango huongeza ubichi kwenye saladi yako.

Endelea kutengeneza viungo utakavyovinyunyuzia kwa juu kwenye saladi. Changanya maembe na juisi ya limau, asali na tangawizi.

Baada ya kuvichanganya, weka kwenye chombo na uongeze majani ya giligilani yaliyokatwa vizuri pamoja na mafuta ya zeituni.

Tingiza kwenye chombo ili vichanganyike vizuri na mara moja. Nyunyuzia kwa juu robo ya mchanganyiko wako kwenye saladi na weka kando.

Kuku

Tayari ulisha-marinate kuku usiku kucha. Changanya viungo – kwa maandalizi ya kuku – vyote na uache vikae kwa dakika 10.

Ondoa kwenye chombo na kwenye kikaangio, mimina mafuta kiasi, kisha weka vipande vya kuku na upike kwa dakika 20, kulingana na unene wa vipande vya kuku.

Epua na ukate vipande vidogovidogo vya kuku. Pakua na ufurahie saladi yako.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Msimu wa tohara ni wakati mzuri kukoleza maadili...

Profesa Oduor: Mifumo ya Bioteknolojia hupitia kaguzi za...

T L