• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:10 PM
MAPISHI KIKWETU: Supu ya viazi mbatata

MAPISHI KIKWETU: Supu ya viazi mbatata

NA MARGARET MAINA

[email protected]

SUPU ya viazi mbatata ni ya kushibisha.

Uzuri wa supu hii ni kwamba ni rahisi sana kuandaa. Mwandaaji anahitaji tu viazi, vitunguu maji, na maziwa.

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji:2

Vinavyohitajika

Viazi mbatata 12

Liki 2 kubwa

Punje 4 za vitunguu saumu

Kitunguu maji 1

Siagi kijiko 1

Vikombe 3 mchuzi wa kuku au mboga

Kikombe ½ cha krimu nzito

Kikombe ½ cha maziwa

Vipandikizi vichache vya kungumanga kwa hiari

Chumvi

Majani ya giligilani

Kitunguu maji. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Chambua na ukate viazi, osha na ukate liki. Ponda vitunguu saumu vizuri. Weka kando.

Kata kitunguu maji, weka kando.

Yeyusha siagi kwenye sufuria na ukaange vitunguu kwa karibu dakika tatu.

Ongeza kitunguu saumu, viazi na kitunguu maji hakafu, koroga vizuri na upike kwa muda wa dakika nane, huku ukichochea mara kwa mara, mpaka mboga iwe laini.

Ongeza supu ya kuku au mboga, funika, chemsha, punguza moto na upike kwa dakika 15-20 au mpaka mboga iwe laini kabisa.

Epua na changanya supu na blenda. Usichanganye sana supu ya viazi na liki au itageuka kuwa gundi.

Unaweza pia kuichanganya kwa sehemu tu na masher ya viazi au kuiacha kama ilivyo.

Ongeza maziwa na krimu na uirudishe motoni tena.

Unaweza kurekebisha ladha na kungumanga, chumvi, na pilipili upendavyo.

Nyunyiza majani ya giligilani zilizokatwa vizuri.

Pakua na ufurahie. Supu ya viazi mbatata.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Viazi vilivyopondwa na kitunguu saumu

Faida za mkaa

T L