• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:50 AM
MAPISHI KIKWETU: Viazi vilivyopondwa na kitunguu saumu

MAPISHI KIKWETU: Viazi vilivyopondwa na kitunguu saumu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

VIAZI vilivyopondwa kwa “instant pot” ni rahisi kutengeneza.

Unaweza kuongeza vipande vya jibini iliyokatwa kwenye viazi na kuongeza krimu chachu.

Ikiwa ungependa kufanya viazi kuwa na viungo kidogo, unaweza kutupa pilipili nyeusi au pilipili ya cayenne.

Badala ya kutumia maji, unaweza kutumia mchuzi wa kuku ili kuongeza ladha zaidi kwa viazi hivi.

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa mapishi: Dakika 10

Walaji: 2

Vinavyohitajika

Viazi mbatata 20

Punje 5 za kitunguu saumu

Vijiko 3 vya siagi isiyo na chumvi

Jibini kikombe ¼

Kijiko 1 cha krimu chachu

Maji kikombe 1  ½

Chumvi

Kijiko 1 cha vipande vya kitunguu kilichokatwa

Viazi kabla ya kutolewa maganda na kuchongwa. PICHA | MARGARET MAINA

Maelekezo

Osha na uchonge ngozi ya viazi. Kata vipande vidogo na uongeze kwenye sufuria ya “instant pot.”

Ongeza kitunguu saumu, siagi kijiko kimoja, chumvi na maji kwenye chungu na ufunike na kifuniko, na uimarishe kisuti cha vali kwenye nafasi ya “kuziba”.

Pika viazi kwa dakika nane kwenye shinikizo la juu.

Mara baada ya mzunguko kukamilika, toa shinikizo iliyobaki mara moja kwa kugeuza kirungu cha vali ya shinikizo kwenye nafasi ya undo ili utoe mvuke.

Ponda viazi kwa mwiko ili viwe laini.

Koroga siagi iliyobaki, krimu chachu, na jibini ya krimu na uongeze kwenye viazi ulivyoponda. Viazi vitakuwa moto na kila kitu kitakuja pamoja na laini.

Hatimaye, ongeza vipande vya kitunguu na upakue viazi. Lakini pia unaweza ukaongezea siagi juu.

Furahia.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Pasta iliyo na mchuzi wa nyanya iliyochomwa

MAPISHI KIKWETU: Supu ya viazi mbatata

T L