• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
MAPISHI KIKWETU: Tambi za karanga za ufuta

MAPISHI KIKWETU: Tambi za karanga za ufuta

NA MARGARET MAINA

[email protected]

BINAFSI ninapendelea siagi ya asili ya karanga kwa sababu haina viungio au vitamu yaani viungo pekee ni karanga na chumvi.

Siagi ya asili ya karanga ina umbile la kioevu zaidi kuliko siagi ya karanga ya kawaida na kwa hivyo itachanganywa kwa urahisi zaidi kwenye mchuzi.

Nyunyiza tambi zilizopikwa na mafuta ya ufuta mara tu baada ya kuosha na kumwaga maji. Hii itahakikisha kwamba tambi hazishikani.

Ikiwa una mzio wa karanga, unaweza kubadilisha siagi ya karanga na badala yake ukatumia siagi ya lozi, siagi ya korosho, au siagi ya alizeti.

Muda wa kuandaa: Dakika 10

Muda wa mapishi: Dakika 30

Walaji: 2

Vinanyohitajika

pakiti 1 ya tambi

vijiko 2 mafuta ya ufuta

vijiko 3 vya siagi ya karanga ya asili

kikombe ¼ cha sosi ya soya

kijiko 1 asali

kijiko 1 siki ya mchele

kijiko 1 kitunguu saumu

kijiko 1 cha mbegu za ufuta zilizokaangwa; kwa ajili ya kupamba (hiari)

vitunguu vya kijani vilivyokatwa; kwa kupamba (hiari)

Maelekezo

Kupika tambi

Kwenye sufuria, chemsha maji juu ya moto mwingi.

Ongeza tambi na upike kwa kufuata maagizo ya kifurushi.

Tambi zikishaiva, mimina maji kwenye sinki, kisha suuza na maji baridi ya bomba hadi tambi ziwe baridi kabisa.

Zihamishe kwenye bakuli la ukubwa wa wastani halafu zichanganye na mafuta ya ufuta kijiko kimoja ili zisishikamane.

Funika kwa karatasi ya plastiki na uziweke kwenye jokofu ili ziwe baridi wakati unatayarisha sosi.

Kuandaa sosi

Katika bakuli ndogo, ongeza kijiko kimoja kilichobaki cha mafuta ya ufuta, siagi ya karanga, sosi ya soya, asali, siki ya mchele na vitunguu.

Changanya kwa uma mpaka kuunganishwa iwe ni laini.

Sasa ongeza kijiko cha maji moto kwenye mchuzi wa ufuta wa karanga kabla ya kuchanganya tambi na sosi pamoja. Unaweza ukala bila kupasha moto. Kipambe chakula hiki na mbegu za ufuta na vitunguu vya kijani ikiwa unataka.

Mabaki yanaweza kuhifadhiwa kwenye chombo kisichopitisha hewa kwenye jokofu kwa hadi siku tatu.

  • Tags

You can share this post!

Mwanawe Ruto atetea ‘afisi ya bintiye rais’

Kunywa juisi uwe na ngozi yenye afya na inayong’aa

T L