• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 2:33 PM
Kunywa juisi uwe na ngozi yenye afya na inayong’aa

Kunywa juisi uwe na ngozi yenye afya na inayong’aa

NA MARGARET MAINA

[email protected]

ILI kuepusha shida zote zinazohusiana na ngozi, na ili ngozi yako ing’ae na iwe na unyevu kutoka ndani, kuna juisi za mboga unazoweza kuziongeza kwenye lishe yako.

Njia bora ya kuufanya mwili wako uwe na unyevu ni kuongezea mboga asubuhi kwa mlo wako wa kifungua kinywa na jioni kabla ya chakula cha jioni. Mwili wako utabaki kuwa na maji na kukufanya ujisikie hai na umechangamka upya.

Juisi ya bitiruti:

Imependekezwa kwa kuwa nzuri kwa utunzaji wa ngozi. Juisi hii hufanya kama kisafishaji kikubwa cha damu, ambayo ni muhimu katika kuweka ngozi yako iwe na mng’ao na yenye afya. Bitiruti pia ina Vitamin C kwa wingi ambayo husaidia na kusawazisha ngozi yako huku ikiipa mng’ao wa asili.

Tango

Juisi ya tango imejaa virutubishi kama vile Vit K, Vit C, magnesiamu, fosforasi, riboflauini, B-6, folate, asidi ya pantotheni, chuma, silika, kalsiamu na zinki. Ndiyo sababu watu wengi huapa kwa kunywa juisi ya tango ili kuweka ngozi zao bila dosari na unyevu kwa muda mrefu.

Nyanya

Juisi ya nyanya husaidia kupunguza kubadilika rangi ya ngozi, husaidia katika kutibu chunusi, kupunguza vinyweleo vilivyo wazi na pia kudhibiti utolewaji wa sebum kwenye ngozi ya mafuta.Kunywa juisi hii mara kwa mara ili kupata wema wote kutoka kwake.

Juisi ya kabeji na tango

Juisi ya kabichi inaweza kukusaidai sana kwa afya ya ngozi yako kwani ina Vitamini C na K na baadhi ya vioksidishaji vinavyolinda ngozi dhidi ya uharibifu. Tumeongeza embe kidogo pia ili kuipa ladha tamu na kuburudisha. Ili kuandaa hii, unahitaji kabichi, majani ya giligilani na tango. Changanya yote pamoja kwenye blenda na hapo utapata glasi ya kuburudisha .

Juisi. PICHA | MARGARET MAINA
  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Tambi za karanga za ufuta

Chakula chenye kiwango wastani cha potasiamu

T L