• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 3:25 PM
MAWAIDHA YA KIISLAMU: Tawakkul ni nguzo muhimu kwa Waislamu wote

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Tawakkul ni nguzo muhimu kwa Waislamu wote

NA HAWA ALI

SIFA zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Subuhaanahu wata’ala, mwingi wa rehema na mwenye kurehemu.

Swala na salamu zimwendee mtume wetu Muhammad swalla Allahu a’alayhi wasallam, swahaba zake kiram na watangu wote wema hadi siku ya kiyamaah.

Moja ya nguzo za kimsingi kwa Waislamu ni dhana ya Tawakkul, ambayo mara nyingi hufafanuliwa kuwa ni imani na kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Kuna tukio kutoka kwa maisha ya Mtume Muhammad swalla Allahu a’alayhi wasallam ambalo linaonyesha mtazamo wazi juu ya Tawakkul.

Siku moja Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimuona ‘bedui’ (Mwarabu wa jangwani) akimwacha ngamia wake bila kumfunga, na akamuuliza yule mtu, “Kwa nini humfungi ngamia wako chini?”

Yule ‘bedui’ akajibu: “Nimeweka imani yangu kwa Allaah.”

Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu swalla Allahu a’alayhi wasallam akasema: “Mfunge ngamia wako kwanza, kisha umtegemee Mwenyezi Mungu.

Tirmidhi – Hii ni Hadith fupi, lakini imebeba somo muhimu kwetu.

Kutokana na majibu ya Mtume Muhammad (SAW), ni dhahiri kwamba mtu huyu hakuelewa kumwamini Mwenyezi Mungu ni nini.

Alifikiri kwamba Tawakkul ilimaanisha kumtarajia Mwenyezi Mungu kuchunga kila kitu bila mtu huyo kuweka juhudi yoyote.

Kwa maneno mengine, ni lazima tufanye sehemu yetu kwanza na matendo yetu kabla ya kuamini kwamba msaada wa Mwenyezi Mungu utakuja.

Ili kuonyesha Tawakkul ya kweli, tunapaswa kufanya sehemu yetu kwanza.

Kwa mfano, ingawa tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mtoa uhai (Al-Muhyi) na Mlinzi/Mhifadhi/Mlezi (Al-Hafidh), inatubidi kuchukua tahadhari za kiafya zinazohitajika ili kujiepusha na maradhi, kama vile kuosha vyombo vyetu, mikono na kufanya mazoezi.

Pia, tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mruzuku (Ar-Razzaq), lakini bado tunapaswa kwenda nje na kuweka juhudi kutengeneza mapato.

Hatutarajii pesa kuanguka tu kutoka angani.

Kwa hivyo, ikiwa wewe au mimi hatufanyi sehemu yetu—ikiwa hatufanyi juhudi kuelekea malengo yetu kupitia matendo yetu, basi hatuonyeshi Tawakkul ya kweli.

Tawakkul maana yake ni kuchukua hatua na kumwamini Mwenyezi Mungu na matokeo ya kitendo chetu

  • Tags

You can share this post!

Ruto awapa Wakenya matumaini

Wanaume watatu kizimbani kwa kuvunja kanisa kuiba viti na...

T L