• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
Naondoka Wizara ya Biashara baada ya kufufua uzalishaji wa viwanda, asema Kuria

Naondoka Wizara ya Biashara baada ya kufufua uzalishaji wa viwanda, asema Kuria

NA WANDERI KAMAU

WAZIRI wa Biashara na Viwanda anayeondoka, Bw Moses Kuria, Ijumaa, Oktoba 6, 2023, alimpokeza rasmi nafasi hiyo waziri mpya, Bi Rebecca Miano.

Bi Miano alihamishiwa katika wizara hiyo mpya na Rais William Ruto kufuatia mabadiliko aliyofanya Jumatano katika baraza lake la mawaziri.

Bi Miano amekuwa akihudumu kama Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maeneo Kame.

Akasema Bw Kuria: “Ninapompokeza Bi Miano Wizara ya Biashara na Viwanda, ninafanya hivyo nikiwa na fahari kubwa sana, kwani kwa muda wa miezi 11 pekee, nimeliwezesha taifa hili kurejea katika uzalishaji wa kiviwanda. Ndoto hiyo inaendelea.”

Bw Kuria alisema kuwa chini ya uongozi wa Rais William Ruto, yuko tayari kuhudumu katika nafasi yoyote atakayopewa.

Licha ya ujumbe huo, wadadisi wa masuala ya siasa walifasiri kuhamishwa kwa Bw Kuria kutoka Wizara ya Viwanda hadi katika Wizara ya Utumishi wa Umma na Uratibu wa Huduma za Serikali kama “kushushwa mamkala” na Rais.

Alipohudumu katika Wizara hiyo, Bw Kuria alijipata pabaya, wakati mwingine hata akikosa kuandamana na Rais Ruto ng’ambo katika masuala yaliyohusu wizara yake.

Mnamo Julai 23, 2023, mwakilishi wa Amerika kuhusu masuala ya kibiashara, Bi Katherine Tai, alifutilia mbali mikutano miwili aliyotarajiwa kufanya na Bw Kuria kujadili mahusiano ya kibiashara baina ya Kenya na Amerika.

Ripoti zilieleza Bi Tai alifutilia mbali vikao hivyo kutokana na matamshi tata ya Bw Kuria dhidi ya watu tofauti na mashirika ya umma.

  • Tags

You can share this post!

Hatujaona hicho chakula cha Sakaja, shule zalia kuhusu...

Kwa nini Uhuru huenda awe mwokozi wa Gachagua mashambulizi...

T L