• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
NDIVYO SIVYO: Ulinganifu wa hali hasi katika methali za Kiswahili

NDIVYO SIVYO: Ulinganifu wa hali hasi katika methali za Kiswahili

NA ENOCK NYARIKI

KATIKA msururu wa makala haya, tumekuwa tukiangazia matumizi mabaya ya baadhi ya methali za Kiswahili.

Tulieleza kuwa yamkini kosa hili husababishwa na kule kufanana kwa maneno fulani kutoka methali moja hadi nyingine – jambo ambalo huwafanya baadhi ya watu kudhani kwamba methali hizo ni visawe.

Mojawapo ya maneno ambayo hujirudia katika baadhi ya methali za Kiswahili, tulivyoeleza wiki iliyopita, ni ‘heri’. Neno hili hubadilishana matumizi na ‘afadhali’ katika ulinganishi wa hali mbili ambapo moja huonekana kuwa bora kuliko nyingine. Mathalani, katika ‘Heri nusu shari kuliko shari kamili’ kuna ulinganishaji wa nusu shari na shari kamili ambapo ‘nusu shari’ inaelekea kuwa afadhali kuliko ‘shari kamili’.

Ingawa baadhi ya watu wanaweza kupinga kuwa mkasa au uovu hauwezi kuwekwa kwenye viwango au kupimwa kwa kutumia vigezo fulani, kwa maoni yangu, jambo hili linayumkinika. Tutaiendeleza hoja hii kwa uketo.

Mwishomwisho wa makala ya wiki jana, tulitaja analojia ya mtu aliyenusurika mauti katika ajali lakini akaishia kupatwa na kilema. Niligusia tu kwamba analojia hii itatusaidia kuelewa jinsi hali zinavyoweza kupimwa kwa vigezo mbalimbali.

Waama, ulinganifu wa hali hasi, kwa mfano, mikosi, uovu, shida na matatizo hudhihirika bayana katika methali kadha za Kiswahili.

Mathalani, katika ‘Maji ya kifuu bahari ya chungu’ unajitokeza ulinganifu wa matatizo ambapo moja linaonekana kuwa kubwa kwa mtu mmoja na likaelekea kumlemea lakini kwa mwingine linaonekana kuwa dogo. Taswira hii pia inasawiriwa na methali ‘Mzigo wa mwenzio…’.

MAKALA YATAENDELEA

You can share this post!

Rovanpera atoa onyo kali katika mpasho Safari Rally ikianza...

VYAMA: Chama cha Kiswahili katika shule ya upili ya Kayole...

T L