• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
NGUVU ZA HOJA: Baadhi ya changamoto zinazokumba makuzi ya Kiswahili Afrika na duniani

NGUVU ZA HOJA: Baadhi ya changamoto zinazokumba makuzi ya Kiswahili Afrika na duniani

NA PROF IRIBE MWANGI

LUGHA ya Kiswahili imekua na kusambaa barani Afrika na ulimwenguni.

Inakadiriwa kuwa na wasemaji zaidi ya milioni 200 duniani.

Kwa hakika, Kiswahili kinasemwa kuwa kati ya lugha 10 zinazotumiwa zaidi ulimwenguni.

Hata hivyo, kuenea kwa Kiswahili kunakumbwa na changamoto kadhaa.

Kwa mfano, Kiingereza hutumiwa kama lugha rasmi katika nchi 27 kati ya 54 zilizoko barani huku nchi 21 zikitumia KiFaransa. Zote mbili ni lugha zilizotumiwa na wakoloni waliotawala mataifa zinamotumika.

Kuondoa matumizi ya lugha hizi na kutumia lugha ya KiaFrika kama kibadala sio jambo rahisi kwa kuwa zimejiimarisha katika matumizi ya kimataifa kwenye diplomasia na bisahara.Barani, kuna lugha zingine zilizoenea.

Kiarabu kimeenea sana Afrika Kaskazini. Katika eneo la magharibi, lugha kama vile KiIgbo, KiHausa na KiYoruba zimeenea sana.

KiYoruba kwa mfano kinasemekana kuwa na zaidi ya wazungumzaji asili milioni 50!

Ili Kiswahili kiweze kukubalika na kukua katika maeneo kama haya, uekezaji wa kifedha na usaidizi wa kisiasa ni muhimu.

Ukubalifu huo utakuwa na manufaa makubwa katika elimu, diplomasia, bishara, utalii, utamaduni, falsafa na siasa.

Ufadhili wa kifedha utasaidia katika kufanya utafiti ili Kiswahili kiweza kutumika katika nyanja zote za maisha.

Pia, ni muhimu mataifa yawe na sera madhubuti za lugha.

Japo jitihada za sasa za kuwa na lugha moja barani Afrika ni muhimu, kufaulu kwa jambo hilo kutawezekana tu ikiwa kuna utambuzi wa changamoto nyingi zilizopo, kujali maslahi ya maeneo mbalimbali na kuwa na mikakati kabambe.

You can share this post!

MAKALA MAALUM: Kutopata ualimu kulimtosa katika utafiti,...

GWIJI WA WIKI: Gladys Mungai

T L