• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
NGUVU ZA HOJA: Yapo matumaini ya kuundwa kwa Baraza la Kiswahili nchini

NGUVU ZA HOJA: Yapo matumaini ya kuundwa kwa Baraza la Kiswahili nchini

NA PROF JOHN KOBIA

MAADHIMISHO ya kwanza ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani yalifanyika wiki jana Julai saba katika sehemu mbalimbali nchini Kenya na kwingineko ulimwenguni.

Wataalamu, wasomi, wanafunzi, maafisa wa serikali, walimu na wakereketwa wa Kiswahili walisherehekea siku hiyo kwa densi, maandamano, nyimbo, mashairi, maigizo, maandishi, kongamano na hotuba mbalimbali.

Watu wengi walitoa wito kwa serikali kuchukua hatua za haraka na za kimakusudi kuunda baraza la Kiswahili la Kenya.

Nampongeza Waziri wa Utalii na Wanyamapori Mheshimiwa Najib Balala kwa msukumo wake wa kutetea Kiswahili.

Yeye na Waziri wa Utamaduni, Turathi na Michezo Balozi Amina Mohamed waliongoza sherehe za maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani jijini Nairobi.

Hatua hii ilifasiriwa kuwa serikali itatilia maanani mchakato wa kuundwa kwa Baraza la Kiswahili la Kenya.

Tamko la Waziri Amina Mohamed kuwa serikali inapanga kubuni baraza hilo lilichangamkiwa sana na wanaoenzi makuzi na maendeleo ya lugha ya Kiswahili.

Wadau wengi wanasubiri kuundwa kwa kamati itakayoendesha mchakato wa baraza la Kiswahili la Kenya baada ya masuala ya kisheria kuzingatiwa.

Baadhi ya majukumu ya baraza hilo yanatarajiwa kuwa kuimarisha na kukuza matumizi ya Kiswahili katika nyanja mbalimbali za maisha kama vile elimu, mawasiliano, dini, siasa, utawala na sharia.

Baraza la Kiswahili la Kenya pia linatarajiwa kushirikiana na vyama vinavohusika na makuzi ya Kiswahili nchini kama CHAKITA na duniani kama CHAKAMA na CHAUKIDU ili kufanikisha maendeleo ya Kiswahili.

Ushirikiano pia unapaswa kuwa baina ya taasisi, vikundi vya watu au hata watu binafsi wanaohusika katika ustawi wa Kiswahili.

  • Tags

You can share this post!

NGUVU ZA HOJA: Ahadi ya Waziri Amina ya kuunda Baraza la...

Mamlaka ya kudadarukia majanga yamulikwa kwa utepetevu...

T L