• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Nzi kufa kidondani si haramu (sehemu ya 3)

Nzi kufa kidondani si haramu (sehemu ya 3)

NA ENOCK NYARIKI

JANJA alikunja uso kama aliyehisi kitefutefu kisha akagogomoka kana kwamba alitaka kutapika.

Janis, alimshukuru Mungu kwa kuwa wateja wengine hawakudiriki kufahamu yaliyoendelea baina yake na Janja.

Mwanamume yule aliinama akavichukua viatu alivyokuwa ameviweka chini ya meza na kuyoyomea nje ya kibanda. Janis alimfuata kwa macho mpaka akatokomea sokoni. Alivichukua vyombo kutoka mezani na kuvipeleka jikoni.

“Jamani hawa nzi si watakuja kutuvurugia biashara!’’ Janis alielezea hisia zake kwa Magiri.

“Kwani kunani tena?’’ Magiri alimwuliza.

“Nzi wengine kwenye chakula cha Janja,’’ Janis alijibu.

“Lakini kwa nini malalamishi hayo hayajawahi kutoka kwa wateja wengine? Ama wao huwaondoa nzi kwenye vitoweo vyao na kuendelea kufurahia?’’ Magiri aliuliza maswali mfululizo.

Swali la kwanza liligonga sikio la Janis kwa nguvu akaliacha lizame moyoni.

Janja alibuni mbinu mpya ili kuhakikisha kwamba biashara aliyoifanya imempa walau vipeni vichache vya kuiwekea aila yake riziki mezani. Chamcha chake alikila mara mbili kwa wiki tena wakati wa siku za soko tu. Siku kama hizo aliwapata wateja wawili watatu ambao walikuwa radhi kumpiga jeki.

Ijumaa mchana, Janja alijituliza kwenye upembe wake wa kawaida kwenye kibanda cha Karibundani.

Tofauti na siku nyingine, Janis hakuwa na haraka ya kumwambia afanye oda hadi Janja mwenyewe alipomwita.

Alihisi kwamba kutochangamkiwa kwake kulitokana na oda ‘hafifu’ alizokuwa na mazoea ya kuzifanya. Aliamua kujishasha: ‘‘Nyama ya makoongo na silesi mbili za ugali.’’

  • Tags

You can share this post!

Nguruwe 4 waangamia baada ya kupigwa na nguvu za umeme...

MWALIMU WA WIKI: Mwalimu mbunifu katika ufundishaji

T L