• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:37 AM
Lojing’i ya Nakuru ambayo haina walevi wala makahaba

Lojing’i ya Nakuru ambayo haina walevi wala makahaba

NA DILIGENCE ODONGO

VYUMBA vya malazi vya gesti na vinginevyo vya kustarehe vinachukuliwa kama ngome za kuendeleza uasherati.

Hata hivyo, marehemu Jeremiah Kibe Muriu, na mkewe Agnes Gachiku Kibe, waliamua kubadilisha kasumba hiyo kwa kujenga vyumba vya gesti vinavyokombolewa na wanandoa tu.

Hakuna anayeruhusiwa kulala katika vyumba hivyo bila kuonyesha ushahidi wa ndoa.

Ushahidi huu unaweza kuwa cheti cha ndoa au vitambulisho vya kitaifa vilivyo na majina yanayolingana, ama pete.

Akizungumza na Mtaa Wangu, meneja wa nyumba hizo Racheal Kibe alisema kwamba, “Tuna sera kali kwa wanandoa kutoa ushahidi wa ndoa kabla ya kuingia. Hii kwa kweli inategemea malezi yetu ya Kikristo yenye msimamo mkali.”

Ilani. PICHA | DILIGENCE ODONGO | MTAA WANGU

Kando na hayo wanandoa hao hawaruhusiwi kuingia katika nyumba hizo baada ya saa sita usiku.

Tofauti na vyumba vingine vya gesti ambavyo hutumika kama maficho ya wanandoa, Bi Kibe alisema vyumba vyao si vyumba vya mipango ya kando.

“Hapa hakuna ukahaba. Hii ni kwa sababu hatuwaruhusu watu walio katika starehe za anasa kukomboa nyumba. Anayekuja hapa sharti aje na mke wake au bwanake,” akaongeza Bi Kibe.

Kwa upande mwingine Bi Kibe anasema kuwa hawaruhusu walevi kukomboa vyumba vyao vya gesti.

“Ulevi au vitu vya ulevi havitakikani. Amani na lazima uimarishwe.”

Waanzilishi wa vyumba hivyo ni waumini ambao wana nia ya kuendeleza injili sio tu kwa matamshi bali pia kwa vitendo.

  • Tags

You can share this post!

Nimripoti mama kwa babangu? Sababu nilimuona akichepuka na...

Kuandaa kahawa ya kupendwa na wateja si...

T L