• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Mwanamuziki Kambua Mathu asimulia pandashuka za maisha akifichua kuhusu idadi kamili ya watoto aliozaa

Mwanamuziki Kambua Mathu asimulia pandashuka za maisha akifichua kuhusu idadi kamili ya watoto aliozaa

NA FRIDAH OKACHI

MWANAMUZIKI wa Injili Kambua Mathu amezungumzia pandashuka zake maishani, akifichua akijifungua watoto wanne na wala si watatu jinsi wengi wanavyojua.

Alifichua hayo katika video yake aliyoichapisha kwenye mtandao wa YouTube.

Kambua anafahamika kuwa mama wa watoto watatu ambao ni Nathaniel, Natalie, na marehemu Malachi.

Lakini kwenye video hiyo, kwa mara ya kwanza amefichua kuwa ni mama wa watoto wanne.

“Wengi wenu mnafahamu nina watoto watatu ambao ni Nathaniel, Malachi ambaye alifariki, na Natalie. Lakini huu si ukweli, nina watoto wanne. Hiki ni kitu ambacho sijawahi kuzungumzia hapo mwanzo, lakini wakati umefika kuwaeleza kuhusiana na malimwengu yangu. Niwaeleze kuhusiana na watoto wawili waliofariki na wawili waliosalia ambao ninawalea,” alisema Bi Kambua.

Katika video hiyo alizungumza kuhusu baba mzazi, Profesa Manundu ambaye alikuwa na mchango muhimu kwenye mahusiano yake wakati wa kuchumbiwa.

“Baba yangu alikuwa rafiki, alikuwa msiri wangu. Baba alikuwa kila kitu… Kuna wakati ambao hatukuelewana kwa kuwa kwenye mahusiano na mtu ambaye nilikuwa nikimpenda sana. Kila wakati baba alikuwa akikataa kuwa huyo mwenzangu hanifai kabisa. Nilitaka kufanya kila kitu kwa uzuri kwa sababu ya baba mzazi,” alisema mwanamuziki huyo.

Kambua alisema alilazimika kuweka ndoto yake ya masomo kando, baada ya kurejea nchini na kufahamu kuwa baba mzazi alikuwa anaugua. Wakati huo alianza kujihusisha na uimbaji na baadaye akafanikiwa kuajiriwa kwenye kituo kimoja cha televisheni.

Pale kazini alifanikiwa kupatana na mchumba wake ambaye kwa sasa ni mume wake.

“Ilikuwa miaka michache ambayo mambo mengi yalifanyika, na wakati huo huo nilitaka ijulikane kuwa iwapo nitafunga ndoa na mchumba wangu, lazima baba awepo. Wakati wa harusi yangu baba alikabiliwa na maumivu. Nilikataa kutoka ndani ya nyumba nikampa baba wakati ili maumivu yaweze kupungua. Baada ya maumivu kupungua alinipeleka mwendo wa aste aste. Nilihisi ndoto yangu imetimia,” alitabasamu kwenye video hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Ruto kutoza ushuru wa juu kwa samaki kutoka China kuwapa...

Ekuru Aukot amshtaki Ruto, ataka hatua kupeleka askari 1,...

T L