• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
PENZI LA KIJANJA: Hizi hapa mbinu za kuteka mumeo asiwe fisi

PENZI LA KIJANJA: Hizi hapa mbinu za kuteka mumeo asiwe fisi

NA BENSON MATHEKA

KWA miaka 15 umekuwa mke mzuri na mwaminifu kwa mumeo.

Kwa heshima zote, unajitolea kumtunza kama mfalme wako ukilenga kuwa na familia yenye furaha lakini unagundua ni mchepukaji hodari.

Unavunjika moyo na badala ya kujirudia, anazidisha tabia yake hadharani na kuianika kwenye mitandao akiwa na vimada ambao hawaheshimu ndoa yako kisha kwa machungu na masononeko unaamua kanuke na kuweka wazi msimamo wako kwamba hauwezi kukubali mke mwenza katika maisha yako.

Na licha ya kutoa msimamo wako huo, mumeo haonyeshi dalili za kubadilisha tabia, huku mpango wake wa kando (na pengine kadhaa) wakimkwamilia kama gundi.

“Haya ndiyo maisha ya kupenda, kuolewa na kuheshimu mtu asiye kupenda. Hata ukimfanyia nini, mtu wa aina hiyo hawezi kubadilika na matokeo yake ni kukuacha na kuchepuka na wanaoteka moyo wake,” asema mwanasaikolojia Levin Kamunge wa shirika la Love Care Nairobi.

“Haitoshi tu kuwa mke mwema, unahitaji kuolewa na mtu anayekupenda kwa dhati. Ni lazima umwelewe mtu wako na kumfanyia asiyoweza kufanyiwa huko nje na kumfanya akutoroke,” asema Levin.

Kuna wanawake wanaotosheka wakiingia katika ndoa na kusahau kwamba wanapaswa kuwajibika zaidi.

“Kukoleza mahaba ni kazi ambayo mwanamke hapaswi kuacha katika maisha ya ndoa. Lazima awe tayari kuimarisha mawasiliano na mumewe. Anapogundua kwamba hapati baadhi ya mambo aliyotarajia katika uhusiano, anapaswa kufungua moyo kwako na usipofanya hivyo ataufungua kwa mtu mwingine anayefanikisha mawasiliano hata kama sio mrembo kama wewe au wa tabaka lake,” asema.

Ni rahisi sana kupenda mtu, asema Deontrae Mayfield katika kitabu chake How to Keep Your Man Faithful, lakini inaweza kuwa vigumu kudumisha mapenzi.

“Hapo ndipo kuna kibarua. Uhusiano wowote bila mapenzi ya dhati kutoka pande zote mbili huwa unatawanyika. Hivyo basi, iwapo unataka kufanya mumeo kuwa wako peke yako, lazima utie bidii kufanya hivyo kwa kumfanyia mambo ambayo wengi wanachukulia kama upuzi,” asema Mayfield.

Wataalamu wa masuala ya ndoa wanasema hakuna kanuni au mwongozo wa mambo ya kumfanyia mumeo ili aweze kubaki mwaminifu kwa uhusiano wa kimapenzi.

“Ni suala ya ubunifu na kuelewa lugha ya mapenzi ya mtu wako, yaani kinachompagawisha, ili uweze kukifanya anavyotaka. Mwache ajihisi kuwa huru na ajieleze kwa maneno na vitendo vyake,” asema mwanasaikolojia Sylvia Smith, akiandika katika tovuti ya www. Marriage.com.

Ili kuzima tabia ya ufisi ya mume kabla ya kuchipuka na kumtawala, Smith anashauri wanawake kuchangamkia tendo la ndoa na kulitia nakshi.

“Unaweza kuwa mke wa kupigiwa mfano na hivyo ndivyo inavyopaswa kuwa, lakini mwanaume akigundua haufurahii kurushana roho, anachukulia kuwa haumpendi na unaweza kufikiria atakachofanya akipata mtu wa kumchangamkia na aliye tayari kumpagawisha wakati wowote,” asema.

Wanasaikolojia wanashauri wanawake kuwa wenye furaha na kukubali waume zao walivyo. Hata hivyo, wanasema kuna ufisi uliopita mipaka wa wanaume ambao hausababishwi na tabia za wake zao.

  • Tags

You can share this post!

MIKIMBIO YA SIASA: Malala atafanikisha ajenda fiche ya Ruto?

Bunge hatarini kuwa mateka wa serikali

T L