• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 8:50 AM
Raila na Kalonzo wapokonywa walinzi

Raila na Kalonzo wapokonywa walinzi

NA SAMMY WAWERU

SERIKALI imewapokonya walinzi vinara wa Azimio la Umoja, katika kile kinaonekana kama kuchochewa na msimamo wao mkali kuhusu maandamano.

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga na mwenzake, Kalonzo Musyoka, Jumatatu, Julai 17, 2023 ilibainika kuwa wamenyang’anywa askari wanaowalinda.

Hatua hiyo pia inajumuisha walinzi wa maboma na makazi yao jijini Nairobi na mashinani.

Kwa sasa, wanategemea walinzi wa kibinafsi.

“Waliondolewa bila notisi,” Bw Opiyo Wandayi, mbunge wa Ugunja aliambia wanahabari katika majengo ya bunge.

Kabla ya tangazo hilo, kiongozi huyo wa wachache bungeni pamoja na viongozi wengine wa kisiasa chama cha ODM waliandaa kikao na wanahabari Nairobi, wakisisitiza kuwa mpango wa maandamano ya siku tatu kuanzia Jumatano, Julai 19 utaendelea licha ya onyo kali la serikali.

Rais William Ruto na Waziri wa Usalama wa Ndani, Prof Kithure Kindiki wamesema hakuna maandamano yatakayofanyika nchini.

Dkt Ruto alisema idara ya usalama itakabiliana vilivyo na waandamanaji.

Azimio inaandaa mandamano kushinikiza serikali ya Kenya Kwanza kushusha gharama ya maisha, pamoja na matakwa mengine ya upinzani.

  • Tags

You can share this post!

Krusedi ya Pasta Ezekiel yafutiliwa mbali Tanzania

Vuguvugu la Operation Linda Ugatuzi laitaka ICC...

T L