• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Saba Saba: Msafara wa Raila Kamukunji wafurushwa na polisi

Saba Saba: Msafara wa Raila Kamukunji wafurushwa na polisi

NA SAMMY WAWERU

MKUTANO wa Azimio la Umoja katika Uwanja wa Kamukunji, Nairobi Ijumaa, Julai 7, 2023 ulilazimika kusitishwa kufuatia hatua ya askari kutawanya wafuasi wa mungano huo kwa kutumia gesi ya vitoa machozi.

Kinara wa muungano huo Bw Raila Odinga, hata hivyo, alikuwa amezungumzia wafuasi wake na kuwajuza baadhi ya viongozi na wanasiasa alioandamana nao.

Mkutano huo ulioshirikisha maandamano yaliyolingana na Sikukuu ya Saba Saba, yanayofanyika Julai 7 kila mwaka.

“Polisi, sisi tunafanya maandamano ya amani. Hatuna ubaya. Msituchokoze,” waandamanaji walisema.

Bw Odinga alitangaza kwamba maandamano yamerejea, hasa baada ya serikali ya Kenya Kwanza kukosa kutii matakwa ya Azimio.

Kabla kukongamana Kamukunji, Odinga alizuru mitaa kadha viungani mwa jiji la Nairobi ambapo alikuwa ameandamana na vinara wenza Kalonzo Musyoka, Martha Karua, Jeremiah Kioni, Wycliffe Oparanya, kati ya wengine.

Wanasiasa hao baadaye walirejea kaunti wanazotoka, kuendeleza maandamano ya Azimio.

“Tunataka serikali ishushe gharama ya juu ya maisha ili kila Mkenya amudu kuishi,” Bw Odinga alisema.

Azimio pia inashinikiza kufunguliwa kwa sava ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kurejeshwa kazi kwa makamishna waliojiuzulu na wengine kufutwa.

Katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2023 ambapo Odinga alimenyana na Rais wa sasa William Ruto (Kenya Kwanza), kesi aliyowasilisha katika Mahakama ya Juu zaidi kupinga matokeo ya urais ilifutiliwa mbali.

Mahakama ilisema haikushawishika na ushahidi uliowasilishwa na kundi la Raila Odinga.

  • Tags

You can share this post!

Ukusanyaji wa saini za kumng’oa Ruto kukamilika wiki...

Saba Saba: Raila Odinga amtaka Rais Ruto kukoma...

T L