• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 9:50 AM
Saba Saba: Raila Odinga amtaka Rais Ruto kukoma ‘kumuibia’ wabunge

Saba Saba: Raila Odinga amtaka Rais Ruto kukoma ‘kumuibia’ wabunge

NA SAMMY WAWERU

KINARA Wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga amemkashifu na kumtaka Rais William Ruto kukoma kuhadaa wabunge wa muungano huo kujiunga na Kenya Kwanza.

Akizungumza Ijumaa, Julai 7, 2023 katika Uwanja wa Kamukunji, Nairobi kiongozi huyo wa upinzani alisema wabunge wa Azimio wanaotaka kujiunga na serikali ya Dkt Ruto wanapaswa kujiuzulu kwanza kabla ‘kusakata ngoma ya Kenya Kwanza’.

Akimsuta Rais Ruto kwa kile alidai anaendeleza njama kudhoofisha upinzani Kenya, alisisitiza wabunge wanaounga mkono sera za serikali yake, Kikatiba wanapaswa kurejea uwanjani kuomba kura kupitia tikiti ya vyama wanavyoshabikia.

“Ni makosa kutuibia wabunge waliochaguliwa chini ya mrengo wa Azimio la Umoja. William Ruto anaenda kinyume na Katiba, akome kupokonya Azimio wabunge,” Bw Odinga aliambia waandamanaji akizungumza Kamukunji Grounds.

Februari 2023, Rais Ruto alialika katika Ikulu baadhi ya wabunge wa muungano wa Azimio hatua ambayo ilionekana kughadhabisha upinzani.

Wabunge hao ni pamoja na Gideon Ochanda (Bondo), Elisha Odhiambo (Gem), Mark Nyamita (Uriri), Caroli Omondi (Suba Kusini), Shakeel Shabir (Kisumu Mashariki) Felix Odiwuor maarufu kama Jalang’o (Lang’ata), Paul Abuor (Rongo), John Owino (Awendo) na seneta wa Kisumu, Tom Ojienda.

Upande wa Dkt Ruto, hata hivyo, ulitetea ziara ya wabunge hao Ikulu, ukisema ililenga kujadiliana umoja wa nchi na maendeleo.

“Tunaambia Bw Ruto, awachane na chama, wachana na Azimio, achana na wabunge wa Azimio…Wakitaka kujiunga na wewe warudi nyanjani wachaguliwe tena kupitia chama chako,” Odinga alisema.

Kenya Kwanza na Azimio; miungano hii miwili ilipimana ubabe wa nani mwenye nguvu wakati wa uidhinishaji Mswada wa Fedha 2023.

Upinzani ulijiunga na wanaokosa mswada huo tata unaopendekeza nyongeza ya ushuru (VAT), ikiwemo ya mafuta ya petroli.

  • Tags

You can share this post!

Saba Saba: Msafara wa Raila Kamukunji wafurushwa na polisi

Mbunge wa Gatanga atoa onyo sharti Del Monte igawe ekari 2,...

T L