• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Shida ya pumu na jinsi unavyoweza kujihadhari nayo

Shida ya pumu na jinsi unavyoweza kujihadhari nayo

NA MARGARET MAINA

[email protected]

PAMOJA na kutumia dawa na mpango sahihi wa matibabu, tiba za nyumbani zinaweza kusaidia kudhibiti dalili za pumu.

Pumu ni hali inayosababisha uvimbe kwenye mkondo wa kupitisha hewa kwenye mapafu. Uvimbe unaosababishwa na kupungua kwa njia ya hewa hufanya iwe vigumu kwa mja kupumua.

Aidha husababisha athari ya kuongezeka kwa kamasi na kukaza kwa misuli karibu na njia ya hewa.

Tiba za nyumbani na matibabu mara nyingi yanaweza kusaidia watu walio na pumu kudhibiti dalili zao za kila siku.

Anayeamua kutumia njia hizi ni sharti afahamu kwamba ni za kusaidia tu mpango wake wa matibabu na wala sio kuzibadilisha.

Mazoezi ya kupumua

Mazoezi ya kupumua mara kwa mara yanaweza kusaidia kupunguza dalili za pumu na kuboresha kwa ujumla hali ya maisha ya watu walio na tatizo hilo.

Ujuzi wa mazoezi ya kupumua ambayo hupunguza uingizaji hewa kupita kiasi yanaweza pia kuwa muhimu wakati wa shambulio la pumu ikiwa mtu hana kipulizia chake mkononi.

Kupunguza dhiki

Mkazo na hisia nyingine kama vile hasira wakati mwingine husababisha shambulio la pumu. Mbinu za kuwasaidia watu kupunguza viwango vyao vya mfadhaiko zinaweza kuwa tiba muhimu za nyumbani kwa anayesumbuliwa na pumu.

Ikiwa mtu hapati kivuta pumzi wakati wa shambulio la pumu, hizi hapa ni baadhi ya mbinu ambazo ni za manufaa kwa mtu kama huyo;

  • kupumua kwa kina
  • kutafakari
  • tiba ya masaji

Kutambua na kuondoa vichochezi

Mojawapo ya tiba bora zaidi za nyumbani kwa pumu ni kutambua na kuondoa vichochezi vya shambulio la pumu. Ingawa hizi zinaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mwingine, baadhi ya vichochezi vya kawaida ni pamoja na;

  • moshi, hasa kutokana na tumbaku, lakini pia kutokana na kuchoma kuni
  • wanyama wa nyumbani, pamoja na paka na mbwa
  • wadudu wa vumbi
  • ukungu
  • uchafuzi wa hewa
  • magonjwa ya kupumua, kama vile mafua
  • hewa baridi

Zaidi ya hayo, kwa watu wengine walio na pumu, mazoezi yanaweza kuzidisha dalili zao, haswa ikiwa wanafanya mazoezi katika hali ya hewa ya baridi.

  • Tags

You can share this post!

Barobaro amsaka Karen Nyamu awe mpenziwe Valentine’s...

Njomo na wabunge wengine wa zamani wa Jubilee waunga mkono...

T L