• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
SHINA LA UHAI: Dalili za ukosaji wa kafeni kwa mraibu

SHINA LA UHAI: Dalili za ukosaji wa kafeni kwa mraibu

NA MARGARET MAINA

[email protected]

KUACHA kafeni kunaweza kusababisha dalili kadhaa, ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa, wasiwasi, kuwashwa, na viwango vya chini vya nishati.

Kupunguza utumiaji wako wa kafeni hatua kwa hatua, kunywa maji mengi, na kupata usingizi mwingi kila usiku kunaweza kuwa na manufaa.

Kafeni ndio inatumiwa sana ulimwenguni ambapo kwa kawaida inapendwa kwa sababu ina kichocheo spesheli kwa mfumo mkuu wa neva, ikimaanisha kuwa inathiri shughuli za neva kwenye ubongo na huongeza tahadhari huku ikipunguza uchovu.

Ikiwa mwili utategemea kafeni, kuiondoa kutoka kwa lishe kunaweza kusababisha dalili ambazo kwa kawaida huanza saa 12-24 baada ya kuacha kuitumia.

Hapa kuna ishara za kawaida zinazohusiana moja kwa moja na mtu kuacha kutumia kafeni.

Maumivu ya kichwa

Maumivu ya kichwa ni miongoni mwa dalili za kukosa kafeni.

Kafeni husababisha mishipa ya damu kwenye ubongo kubana, hali ambayo hupunguza mtiririko wa damu. Matumizi ya kafeni husababisha mishipa ya damu kuwa myembamba hivyo kupunguza au kuacha utumiaji huruhusu mishipa ya damu kufunguka na kuongeza mtiririko wa damu kwenye ubongo. Mabadiliko haya ya ghafla ya mtiririko wa damu yanaweza kusababisha maumivu ya kichwa.

Uchovu

Watu wengi hutegemea kikombe cha kahawa kila siku ili kuwapa nguvu zaidi.

Kafeni husaidia kuongeza tahadhari na kupunguza uchovu kwa kuzuia vipokezi vya adenosine, nyurotransmita inayoweza kukufanya uhisi kusinzia. Lakini kuondoa kafeni kutoka kwa lishe yako kunaweza kuwa na athari tofauti ikiwa ni pamoja na kusababisha usingizi na uchovu.

Wasiwasi

Kafeni ni kichocheo ambacho mara nyingi kinaweza kuongeza mapigo ya moyo na shinikizo la damu. Kwa baadhi ya watu, kikombe kimoja tu cha kahawa kinaweza kuwafanya wahisi kutetemeka na kuwa na wasiwasi. Ingawa kutumia kafeni kunaweza kusababisha hisia za wasiwasi, kuacha kunaweza kusababisha athari hii pia.

Ugumu wa kuwa makini

Mojawapo ya sababu kuu ambazo watu huchagua kutumia kafeni kwa njia ya kahawa, chai, au vinywaji vya kuongeza nguvu ni kuongeza umakini.

Mchanganyiko huu wa athari huongeza kiwango cha mapigo ya moyo na shinikizo la damu na kuchochea ubongo, na kusababisha kuongezeka kwa tahadhari na kuboresha umakini. Kuondoa kafeni kunaweza kuathiri vibaya umakini wakati mwili wako unajitahidi kuzoea kufanya kazi bila.

Hali ya huzuni

Kafeni inajulikana sana kwa uwezo wake wa kuinua hisia. Uwezo wa kuzuia adenosine sio tu huongeza tahadhari, lakini pia kuboresha au kuimarisha hisia. Watu wanaotumia kahawa yenye kafeini wanapata uboreshaji wa hali ikilinganishwa na wale wanaotumia kahawa isiyo na kafeni.

Nishati ya chini

Kila mtu anayetumia vinywaji na vyakula vyenye kafeni anatafuta njia ya kuboresha viwango vya nishati. Mambo ya mtindo wa maisha kama vile usingizi duni, kazi nyingi na lishe isiyofaa yanaweza kumaliza nishati na kusababisha watu wengi kufikia vyanzo vya nje vya nishati kama vile kahawa na vinywaji vya kuongeza nguvu ili kuwapa nguvu. Vinywaji vilivyo na kafeni mara nyingi hutumiwa kama njia ya kutolea nishati inayohitajika ili kuifanya siku nzima au kufidia ukosefu wa usingizi.

You can share this post!

Matumizi mbalimbali ya zaatari almaarufu Thyme

Kalonzo pabaya Ruto akiweka mikakati kupenya ngome yake

T L