• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
SIHA NA LISHE: Tunda la chenza

SIHA NA LISHE: Tunda la chenza

NA MARGARET MAINA

[email protected]

CHENZA ni tunda la jamii ya chungwa lenye ganda laini. Hivyo ni rahisi kulimenya tunda hili.

Kwa kawaida huwa na umbo dogo kuliko chungwa.

Unaweza kula chenza jinsi lilivyo, au ukalitumia tunda hili kutengeneza juisi ya kuburudisha, au ukalitumie kutengeneza jamu tamu au likatumika kwenye saladi.

Tunda aina ya cheza limesheheni virutubisho

Licha ya saizi yake ndogo ikilinganishwa na matunda mengine ya jamii ya chungwa, chenza huwa na maji ya kutosha na virutubisho kama vile kalori, wanga, nyuzinyuzi, protini, mafuta, potasiamu na vitamini C na A.

Kwa kawaida chenza huwa na maji matamu na nyuzinyuzi. PICHA | MARGARET MAINA

Kuimarisha mfumo wa kingamwili

Vitamini C katika chenza husaidia kulinda mfumo wako wa kinga dhidi ya virusi na bakteria kwa kutenda

Kwa kuongezea, vitamini C huongeza seli za kinga ambazo humeza bakteria na vimelea hatari – na kuua vijidudu, hali inayoimarisha mwitikio wako wa kinga.

Inaweza pia kusaidia kupunguza ukali wa athari za mzio.

Kuboresha mwonekano wa ngozi

Kuongeza chenza kwenye lishe yako kunaweza kusaidia na kufanya ngozi ya mlaji iwe yenye afya kwa sababu ya athari ya vitamini C kwenye utengenezaji wa kolajeni.

Kolajeni ni protini muhimu zaidi katika mwili. Mja akizeeka kiasi cha kolajeni katika mwili hupungua. Hata hivyo, vitamini C inakuza usanisi wa kolajeni, ambayo huboresha uponyaji wa jeraha na kupunguza dalili za kuzeeka, kama vile mikunjo na makunyanzi.

Kupunguza uzito

Anayekula chenza akitaka matokeo ya kupoteza uzani huwa hajafanya kazi bure kwani matunda ya jamii ya machungwa, ikiwa ni pamoja na chenza, hutoa nyuzinyuzi zisizoyeyuka – aina ambayo haichachi kwenye utumbo.

Aina hii ya nyuzi huongeza hisia za ukamilifu kwa kupunguza kasi ya usafiri wa chakula kupitia njia yako ya utumbo. Hii nayo husaidia kudhibiti hamu yako ya kula, ambayo inaweza kuimarisha safari ya kukata uzani.

Zaidi ya hayo, watu walio na mazoea ya kula chakula chenye nyuzinyuzi wanaweza kudumisha uzani wao wa mwili au kuzuia kupata uzito tena ikilinganishwa na wale wanaokula chakula chenye nyuzinyuzi kidogo.

Rahisi kuongeza kwenye lishe yako

Chambua na ukate sehemu kisha uongeze kwenye saladi

Kamua ili upate juisi ya chenza

Tengeneza salsa safi ya chenza kufurahia na samaki au kuku.

Ongeza kwenye mtindi au chia kwa kiamsha kinywa chenye lishe au vitafunio

Kwa ujumla, chenza mbichi hazihitaji kuwekwa kwenye jokofu. Hata hivyo, ikiwa unataka kuzimenya kabla ya wakati, hakikisha unahifadhi chenza kwenye chombo ndani ya jokofu.

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa wa ujambazi ashtakiwa kwa kudai fidia ya Sh1.9...

Vidokezo mahususi kwa vijana kupunguza uzani

T L