• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Sofia: Sijapata nafasi lakini sitavunjika moyo

Sofia: Sijapata nafasi lakini sitavunjika moyo

Na JOHN KIMWERE

NI ndoto ya kila msanii kuona anaimarika katika kazi zake na kutambulika pia kukubalika kote duniani.

Purity Syongo maarufu Sofia aachwi nyuma ameorodheshwa kati ya kina dada wanaoendelea kujituma kiume katika tasnia ya maigizo huku wakipania kutinga hadhi ya kimataifa miaka ijayo. Ingawa hajapata nafasi ya kutamba tangia aanze kujituma kwenye sekta ya uigizaji mwaka 2018 anasema kuwa anatosha mboga.

”Taifa hili nimefurika wasanii wengi tu wanaume kwa wanawake ambao hajafanikiwa kupata nafasi za kuonyesha ujuzi wao,” alisema na kuongeza anafahamu kuwa ipo siku atakubalika. Kando na uigizaji dada huyu ni mwanabiashara. Binti huyu aliyezaliwa mwaka 2000 anasema alianza kushiriki uigizaji kupitia kundi la Strong Pillarz Entertainment.

Pia amefanya kazi na kundi liitwalo GJ Production Mwanzo anadokeza alivutiwa na masuala ya uigizaji baada ya kutazama msanii Tanya alivyokuwa akifanya kwenye kipindi cha Tahidi High kilichokuwa kikipeperushwa kupitia runinga ya Citizen TV.

Binti anajivunia kushiriki vipindi kadhaa tangia mwaka 2018 ikiwamo: Closure na Perfect Match zote Ebru TV, Auntie Boss (Maisha Magic) Nisamehe (KTN) pia filamu fupi Black Tears (K24) kati ya zinginezo. Kwa kazi zake anasema anapenda jinsi alivyofanya kwenye kipindi cha Auntie Boss. Anasema kwa jumla katika uhusika wake amefanya kazi nzuri katika kipindi hicho.

Purity Syongo maarufu Sofia…Picha/ JOHN KIMWERE

Anasema Afrika angependa kufanya kazi nao Mercy Johnson mwigizaji wa filamu za Kinigeria (Nollywood) pia Wema Sepetu msanii wa Bongo Muvi.

Mercy ameshiriki filamu nyingi ikiwamo ‘The maid,’ ‘Heart of a fighter,’ ‘Hustlers,’ ‘Keziah,’ na ‘The leged of inikpi,’ kati ya zingine. Hapa nchini anasema angependa kufanya kazi na wasanii kama Tanya mhusika mkuu katika kipindi cha Zora ambacho hupeperushwa kupitia Citizen TV. Tanya pia alikuwa kati ya walioshiriki kipindi cha Tahidi High.

Tangia akiwa mtoto dada huyo alitamani kuhitimu kuwa wakili pia kuwa mwigizaji tajika duniani. ”Ingawa sijapata mashiko bado sijavunjika moyo nina hamu ya kushiriki kazi za viwango vya kimataifa miaka ijayo,” alisema na kutoa wito kwa serikali ianzishwe kumbi nyingi mashinani ili kutoa nafasi kwa vijana kushiriki mazoezi ya masuala ya uigizaji. Anadokeza kuwa serikali za Afrika Kusini na Nigeria kwa asilimia fulani zimepatia uigizaji kupau mbele hali ambayo umechangia sekta hiyo kupiga hatua zaidi hasa kwa kutoa nafasi za ajira.

CHANGAMOTO

Kiukweli wengi wetu tunapitia wakati mgumu kukosa ajira ya uigizaji. ”Binafsi nimeshiriki majaribio mara nyingi tu ila hukosa kupata nafasi hali ambayo huchangia kujikuta pabaya kwa njaa,” akasema. Anashauri wenzake kuwa wasikate tamaa maana sekta ya uigizaji inahitaji subira pia wanadada wasitumie mwili wao kujipatia ajira.

You can share this post!

Berita: Upshaws yazidi kumpa umaarufu katika uigizaji

VALENTINE OBARA: Kaunti idhibiti vilivyo uchimbaji visima,...

T L