• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
SOKOMOKO WIKI HII: Cherera alivyopiga chenga Wakenya kwa ‘mahesabu ya ajabu’

SOKOMOKO WIKI HII: Cherera alivyopiga chenga Wakenya kwa ‘mahesabu ya ajabu’

NA CHARLES WASONGA

WIKI hii Naibu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Juliana Cherera aliwapa Wakenya zoezi gumu la hisabati la kubaini dosari katika hesabu za matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotolewa na bosi wake Wafula Chebukati.

Huku akiwa ameandamana na makamishna wenzake watatu waliojitenga na matokeo yaliyotangazwa na Bw Chebukati, Bi Cherera alidai kuwa kasoro ya asilimia 0.01 katika hesabu hizo iliwakilisha jumla ya kura 142,000.

“Idadi hii ya kura ingeleta mabadiliko makubwa katika matokeo ya ya mwisho. Hii ni kwa sababu kwa kujumuisha asilimia 48.85 za Raila Odinga, asilimia 50.49 za William Ruto, asilimia 0.27 za Waihiga Mwaure na asilimia 0.44 za Profesa George Wajackoyah unapata asilimia 100.01. Asilimia 0.01 za juu ni sawa na kura 142,000 ambazo Chebukati hajatueleza zilikokwenda,” akawaambia wanahabari katika mkahawa wa Serena, Nairobi.

Alirejelea kauli hiyo katika maelezo ya ziada baada ya kusoma taarifa yake rasmi, kuashiria kwamba haikutokana na kuteleza kwa ulimi.

Ghafla bin vuu, Wakenya katika mitandao ya kijamii na wahabari waligundua kosa katika hesabu za Bi Cherera.

Ilibainika kuwa, naibu mwenyekiti huyo wa IEBC alinoa katika ukadiriaji wake wa idadi ya kura zinazowakilishwa na asimilia 0.01 ya idadi jumla ya kura za urais.

Walioshiriki zoezi la ukadiriaji huo, kwenye mitandao ya kijamii na katika vyombo rasmi vya uchaguzi, waliafikiana kuwa idadi halisi ni kura 1,420.

Bi Cherera, alielekezewa lawama tele kwa kuwapotosha Wakenya na walimwengu.

  • Tags

You can share this post!

Zaha aongoza Crystal Palace kuzamisha Aston Villa ligini

WALIOBOBEA: Akaranga alivyobadilisha sekta ya umma nchini

T L