• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
WALIOBOBEA: Akaranga alivyobadilisha sekta ya umma nchini

WALIOBOBEA: Akaranga alivyobadilisha sekta ya umma nchini

KWA HISANI YA KENYA YEAR BOOK

MOSES Akaranga, mtaalamu wa Benki aliyebadilika kuwa kasisi, anakumbukwa kwa kuanzisha kandarasi za kazi na utendaji alipoteuliwa Waziri wa Utumishi wa Umma mwaka wa 2006.

Pia, alisimamia kuchunguzwa kwa mishahara na pensheni katika sekta yote ya utumishi wa umma.

Jukumu lake la kwanza baada ya kuteuliwa waziri lilikuwa ni kupata imani miongoni mwa uongozi wa vyama vya watumishi wa umma ambayo ilikuwa imedorora chini ya uongozi wa mtangulizi wake William ole Ntimama, ambaye vyama vilisema hakujali maslahi ya watumishi wa umma

Hii pengine inaeleweka ikizingatiwa kwamba alipenda sana kuwalaumu katika mikutano a ya kisiasa badala ya mikutano ya ofisini.

Kwa upande wake, Akaranga alikuwa msimamizi wa biashara aliyebobea kando na kutaja maisha yake kama Msimamizi Mkuu wa Kanisa la Pentecostal Assemblies of God, aliyezoea mazungumzo na kukubali mikataba.

Kuhudumu kwake katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni kama Katibu Msaidizi, Naibu Katibu na Kaimu Katibu wa Wizara bila shaka kulijenga na kuimarisha ujuzi wake wa diplomasia.

Akiwa na digrii ya Uzamili katika usimamizi wa biashara kutoka chuo Kikuu cha Kimataifa cha Amerika na digrii ya Uzamifu katika upangaji wa mikakati kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, mtindo wa Akaranga ulijenga mazungumzo badala ya vitisho na akabadilisha utumishi wa umma kutoka mizozo ya kortini na maandamano hadi mazungumzo ya kutatua mizozo hiyo.

Mbinu hizi mpya za mawasiliano zilizaa mishahara mipya kwa wafanyakazi wa chini hadi wa vyeo vya juu katika utumishi wa umma.

Kabla ya kuteuliwa waziri, kulikuwa na malalamishi kwamba serikali ilikuwa ikijali maslahi ya wafanyakazi wakuu na wa vyeo vya kati katika utumishi wa umma na kupuuza wale wa viwango vya chini ambao ndio wengi.

Matunda ya juhudi zake yalikuwa motisha hasa kwa wafanyakazi wa vyeo vya chini hatua ambayo iliongeza bidii na uzalishaji.

Akaranga aliajiri wataalamu 100 wa wafanyakazi kutathmini na kutayarisha viwango vya wafanyakazi, nafasi zilizopaswa kujazwa na masomo na ujuzi uliohitajika.

Kwa kutumia ripoti hiyo, serikali ilipata mwongozo wa uajiri wa wafanyakazi.

Idara ya Usimamizi wa Wafanyakazi pia ilifanyiwa mageuzi ili kuajiri, kutoa mwongozo wa ajira na kufanya utathmini. Chini ya Akaranga, wafanyakazi wa serikali pia walihimizwa na kuwezeshwa kurudi shule kupata maarifa zaidi na ujuzi waweze kuendeleza na kukua katika kazi zao.

Kwa mara ya kwanza tangu uhuru, wafanyakazi kazi wengi zaidi wa umma walirudi masomoni wakati wa utawala wa Kibaki wakiwemo kutoka vikosi vya usalama kama jeshi la Kenya na polisi.

Serikali iliwapa watumishi wa umma likizo ya masomo na pia kuwatunza wale waliokuwa na masomo ya juu kwa kuwapandisha vyeo.

  • Tags

You can share this post!

SOKOMOKO WIKI HII: Cherera alivyopiga chenga Wakenya kwa...

Naibu rais ajaye kuvumilia bajeti

T L