• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 10:50 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Aden Duale asije akasahau haki ya marehemu Agnes Wanjiru

TUSIJE TUKASAHAU: Aden Duale asije akasahau haki ya marehemu Agnes Wanjiru

MNAMO Novemba 2, 2021 aliyekuwa Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa alitoa hakikisho kwamba Serikali ya Uingereza imekubali kushirikiana na Kenya kufanikisha kukamatwa na kuadhibiwa kwa mwanajeshi wa Uingereza aliyemuua Agnes Wanjiru mjini Nanyuki, Kaunti ya Laikipia.

Bi Wanjiru, 21, alipatikana ameuawa katika mkahawa mmoja mjini humo mnamo Oktoba 12, 2012 baada ya kuonekana mara ya mwisho akiwa na mwanajeshi mmoja wa Uingereza.

Bw Wamalwa aliambia Kamati ya Bunge kuhusu Ulinzi na Masuala ya Kigeni, kwamba alipata hakikisho, wakati huo, kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace, kwamba “mshukiwa huyo atakamatwa”.

Lakini alikimya kuhusu suala hilo hadi alipoondoka afisini juzi.

Kwa hivyo, Waziri mpya wa Ulinzi, Aden Duale asije akasahau kushughulikia suala hilo ili familia ya marehemu Wanjiru ipate haki, ambayo imecheleweshwa kwa miaka 10.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Wahamiaji walivyogeuza mkondo wa siasa...

TAHARIRI: Mashauriano na maelewano yatamalaki FKF ikianza...

T L