• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:50 AM
MAWAIDHA YA KIISLAMU: Umuhimu wa vazi la hijabu kwa mwanamke Mwislamu

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Umuhimu wa vazi la hijabu kwa mwanamke Mwislamu

NA HAWA ALI

SIFA zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Subuhaanahu wata’ala, mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu.

Swala na salamu zimuendee mtume wetu Muhammad Swalla Allahu a’alayhi wasallam, Swahiba zake jirani na watangu wote wema hadi siku ya kiyama.

Hijabu inayotakiwa kisheria ni mwanamke kufunika sehemu zote za mwili wake zilizokuwa haramu kuonekana wazi, au kusitiri sehemu zote za mwili wake ambazo ni wajibu kwake kusitiri.

Kuna dalili mbali mbali kutoka kwenye kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna sahihi za Mtume wake Swalla Allahu a’alayhi wasallam na maneno ya maswahaba na maneno ya wanazuoni wa Kiislamu na maimamu wake yenye kuonyesha kwamba ni wajibu kwa mwanamke wa kiislamu kusitiri sehemu zote za mwili wake mbele ya watu wasiokuwa maharimu wake. Kisha kumruhusu mwanamke kutoa uso na viganja vya mikono yake.

Mwenyezi Mungu Subuhanahu wata’ala anawaamrisha waislamu wanawake wajistri nguo ya juu isiobana wakati wakitoka nje. Kwa kufanya hivi watatofautishwa na wasiokuwa waislamu na wanawake wengine viruka njia.

Mwenyezi Mungu Subuhanahu wata’ala alimwamrisha mtume wake Swalla Allahu a’alayhi wasallam awaambie umma wa Kiislamu ujumbe huu kutoka kwake: Ewe mtume! Waambie wake zako, na binti zako na wanawake wa Kiislamu, wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane kuwa ni watu wa heshima ili wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni msamehevu na mrehemevu. (33:59)

Na kaeni majumbani mwenu, wala musionyeshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionyesha mapambo yao wanawake wa zama za jahiliya.(33:33)

Mtume amesema, “Mwanamke avuae nguo (akawa uchi) ikiwa si nyumbani kwa mumewe basi huwa kararua pazia (sitara) baina yake na Mola wake. (Tirmidhi) pia amesema “katika wakaazi wa motoni watakuwako wanawake ambao watakuwa wamevaa nguo lakini wako uchi. Wanatongoza na wanatongozwa. Hawa hawataingia peponi na hata harufu yake hawatainusa.”

  • Tags

You can share this post!

Kamishna Mkuu wa KRA, Mburu ajiuzulu

KIKOLEZO: Maisha na mikasa ya nguli Tedd Josiah

T L