• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
WALLAH BIN WALLAH: Asanteni ndugu Watanzania kwa kunitambua na kunituza kwenye maadhimisho ya Siku ya Kiswahili jijini Dar

WALLAH BIN WALLAH: Asanteni ndugu Watanzania kwa kunitambua na kunituza kwenye maadhimisho ya Siku ya Kiswahili jijini Dar

NA WALLAH BIN WALLAH

NDUGU wapenzi wa Kiswahili, sina nia ya kujisifu wala kujipigia upatu! La hasha!

Ninayaandika makala haya ili kuwadokezea tu furaha niliyo nayo kwamba kwenye sherehe zilizofana zaidi jijini Dar es Salaam Tanzania tarehe saba Julai wakati wa kuadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani kwa maandalizi ya Serikali ya Tanzania, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania (BAKITA), nilituzwa tuzo adhimu zaidi kutokana na walivyosema kuwa Mdau Mwenye Mchango Mkubwa wa Kiswahili Afrika Mashariki!

Imenibidi kuwataarifu tukio hili teule kudhihirisha furaha zangu moyoni kwa kupokea tuzo hii niliyotuzwa kwenye hafla kubwa wakati muhimu mno walimwengu wote walipokuwa wakiadhimisha kwa mara ya kwanza Siku ya Kiswahili Duniani tangu Shirika la UNESCO lilipotangaza na kuidhinisha sherehe hizo zifanyike.

Ninaomba kwa heshima na unyenyekevu kuwashukuru kwa dhati ya nafsi yangu Ndugu Watanzania kwa kunitambua na kuteua kunituza miongoni mwa watu mashuhuri waliotuzwa siku hiyo katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam Tanzania.

Shukrani za pekee zimfikie Dkt. Consolata Mushi Katibu Mtendaji aliyenitumia mwaliko rasmi kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo pamoja na Sekretarieti ya BAKITA!

Asanteni sana nyote!

Ni dhahiri shahiri kwamba mtu mchache wa fadhila ndiye awezaye kupuuza kumshukuru aliyemtendea wema! Kwani kuendako hisani hurudi hisani hakurudi nuksani! Fadhila hulipwa kwa fadhila; hailipwi kwa ufidhuli!! Mungu awabariki!

  • Tags

You can share this post!

Wanawake 30 wafanya ujima kujiendeleza kwa mtambo wa kusaga...

BITUGI MATUNDURA: Siku ya Kiswahili Duniani ina mawanda...

T L