• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 7:55 PM
BITUGI MATUNDURA: Siku ya Kiswahili Duniani ina mawanda mapana kuliko ya Waswahili kindakindaki

BITUGI MATUNDURA: Siku ya Kiswahili Duniani ina mawanda mapana kuliko ya Waswahili kindakindaki

NA BITUGI MATUNDURA

MAADHIMISHO ya Siku ya Kiswahili Duniani mnamo Alhamisi 7, juma lililopita – kuitikikia wito wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yalifana mno.

Hafla hiyo ilitoa fursa kwa wadau wa Kiswahili kutafakari mustakabali na mikondo na maendeleo ya Kiswahili siku za usoni.

Motifu iliyotawala hafla hiyo ni kongamano la mawazo kwamba, Kiswahili ni lugha muhimu ulimwenguni, inayopaswa kukuzwa kimakusudi kama chombo cha kuimarisha ushirikiano, mawasiliano na mtagusano wa jamii.

Aidha ipo haja ya kubidhaaisha Kiswahili kwa minajili ya maslahi ya kiuchumi.

Nchini Kenya, hafla hiyo ilitoa fursa murua ya wataalamu wa Kiswahili kuidara Serikali, ichapushe mchakato wa kubuni Baraza la Kiswahili la Kenya (BAKIKE), ambao umekwama kwa muda mrefu.

Hali hiyo imechangiwa na ukosefu wa msukumo wa kisiasa. Masuala kuhusu sera ya lugha ni ya kisiasa.Hafla hiyo pia ilizua midahalo kadha.

Mtaalamu na msomi, Prof Rocha Chimerah kwa mfano, alieleza kwa kina chanzo cha baadhi ya lugha, kikiwemo Kiswahili, kuwa na leksikoni kadha za Kiarabu.

Lugha hizo ni pamoja na: Kiturki (asilimia 50), Kibengali, Kiurdu, Kijavanese (asilimia 60), Pushkin n.k.

Lugha iliyotumika kueneza dini ya Uislamu ilikuwa ni Kiarabu.

Kiswahili kina asilimia 30 ya maneno ya Kiarabu.

Rai kwamba Kiswahili hivi sasa ni lugha ya jamii fulani (wasemaji kindakindaki) huenda haina manufaa makubwa sana, kwa misingi kuwa, sasa ni lugha ya kiulimwengu kama vile Kiingereza. Imekwisha kutoka katika mawanda hayo.

  • Tags

You can share this post!

WALLAH BIN WALLAH: Asanteni ndugu Watanzania kwa kunitambua...

NGUVU ZA HOJA: Ahadi ya Waziri Amina ya kuunda Baraza la...

T L