• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 12:17 PM
CHARLES WASONGA: Kalonzo alisaliti Mudavadi, Wetang’ula kuweka siri mkataba wake na Raila

CHARLES WASONGA: Kalonzo alisaliti Mudavadi, Wetang’ula kuweka siri mkataba wake na Raila

NA CHARLES WASONGA

UNAPOMWELEKEZEA mwenzako kidole kimo – ja ukimlaumu kwa jambo fulani, usisahau kuwa vidole vilivyosalia vinaelekea kwako, yaani wewe pia haukosi doa.

Kimsingi, unapomlaumu mwenzako kwa kukukosea au kukusaliti kwa njia moja ama nyingine, kumbuka wewe sio “mweupe kama pamba”. Kuna uwezekano mkubwa kuwa umewahi kuwetendea wengine mabaya yayo hayo unayodai mwenzako alikutendea.

Ungama kwanza kabla ya kurusha kombora la lawama. Katika mukhtada huu, ningependa kumshauri kiongozi wa Wiper, Stephen Kalonzo

Musyoka kwamba, japo ana haki ya kulalama kwamba kiongozi wa ODM Raila Odinga amemsaliti kwa kukosa kutimiza ahadi ya kumuunga mkono kwa kiti cha urais 2022, yeye (Kalonzo) pia amewahi kuwachezea shere wanasiasa wenzake.

Jumatano, Bw Musyoka alifichua kwamba, yeye na Bw Odinga walitia saini makubaliano ya kisiri kwamba, baada ya kumuunga mkono kiongozi huyo wa ODM kama mgombeaji urais wa uliokuwa muungano wa NASA katika uchaguzi mkuu wa 2017, Bw Odinga angemuunga mkono kuwania wadhifa huo 2022. Kwa hivyo, makamu huyo wa rais wa zamani anashikilia kuwa yuko tayari kujiunga na vuguvugu la Azimio la

Umoja japo kwa sharti kwamba, Bw Odinga amuunge mkono kama mwaniaji wa urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9, mwaka huu. Lakini sasa imefichuka kwamba, vinara wengine wa NASA, wakati huo, Mbw Musalia Mudavadi (kiongozi wa ANC) na Moses Wetang’ula (Ford –Kenya) hawakuwa na habari kuhusu uwepo wa mkataba huo, kati ya Mbw Musyoka na Odinga.

Kwa hivyo, tasnifu yangu ni kwamba kwa kutowajuza Mbw Mudavadi na Wetang’ula, kuhusu mkataba wa kwanza kati yake na Bw Odinga, Bw Musyoka pia aliwasaliti viongozi hao wa ANC na Ford Kenya.

Alitenda dhambi ambayo sasa anadai Bw Odinga alimtenda.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Uhuru hafai kutumia lugha ya mama katika...

Nilimnoa kisiasa Ruto na haniwezi, Raila sasa ajigamba

T L