• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
JUMA NAMLOLA: Serikali iboreshe uchukuzi wa umma kuokoa maisha ya waendao Krismasi

JUMA NAMLOLA: Serikali iboreshe uchukuzi wa umma kuokoa maisha ya waendao Krismasi

Na JUMA NAMLOLA

SIKU kama ya leo wiki ijayo, mamilioni ya waumini wa dini ya Kikristo kote ulimwenguni watakuwa kwenye mkesha wa siku ya Krismasi.

Umuhimu wa siku hii haufananishwi na siku nyingine kwenye kalenda.

Kama kungekuwa na nafasi ya kuipa jina, hapa Kenya Krismasi ingeitwa ‘Siku ya kuzuru mashambani’.

Wakenya wengi waliotokomea mijini na kuzongwa na shughuli, hutumia fursa hii ya mapumziko ya karibu wiki moja, kusafiri kwenda kwao mashambani.

Watoto waliozaliwa na kukulia mijini kama Nairobi, huanza kuita ng’ombe (nyati).

Kuna wengi watakaorejea mijini wakiwa na majeraha ya kuangushwa na mbuzi beberu kwa kujaribu kushikilia kamba yake.

Wengi wanaosafiri mashambani msimu huu, watajaribu kuambukiza watu wa mashambani lahaja na lafudhi ya mijini, kuongea kwa king’ong’o (puani), kutumia ‘niaje’ na kubeba maji ya chupa.

Hizo ni changamoto za kuishi mijini, na kuna umuhimu mkubwa kwa walio na uwezo, kuwaonyesha watoto wao kuwa kuna maisha ya kuoga kwa kujimwagia maji kwa kopo, badala ya kusimama chini ya shawa, na kadhalika.

Ziara hizi za kwenda mashambani, yafaa zitumike kuwafunza watoto wetu kwamba maisha, kama ilivyo safari, yana pande mbili.

Sababu hasa ya kuangazia safari za mashambani ni usafiri wa kuwafikisha na kuwarejesha watu salama salimini.

Takwimu za mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA), zinaonyesha kuna ongezeko la ajali na vifo barabarani mwezi huu wa Disemba.

Tayari zaidi ya watu 200 wamekufa tangu mwezi huu uanze. Hii si idadi ndogo. Hata mtu mmoja haifai afe barabarani.

Kwa wanaoeleka magharibi ya nchi, Shirika la Reli limeanzisha garimoshi kwa bei nafuu. Kinachohitajika ni kuboresha safari hizo, ili wengi wanaotaka kusafiri, wapate njia mbadala ya kuwafikisha mashambani.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Mvutano wa Mahakama, Afisi ya Rais hatari...

Viongozi wa Chadema wakataa kikao na rais

T L