• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:50 AM
KINYUA KING’ORI: Serikali ikome kuongeza ushuru mpya kwa raia wanaoumia tayari

KINYUA KING’ORI: Serikali ikome kuongeza ushuru mpya kwa raia wanaoumia tayari

NA KINYUA KING’ORI

RAIS William Ruto na viongozi wengine katika serikali ya Kenya Kwanza inaonekana wamesahau Wakenya waliwachagua kwenye uchaguzi mkuu uliopita kwa sababu walikuwa wamechoshwa na serikali isiyojali maslahi yao.

Serikali hiyo ilikuwa ikiwatoza ushuru na pia bidhaa muhimu kiasi cha kusongwa na gharama ya maisha yao.

Tunajua kulipa ushuru ni wajibu wetu na ili serikali kupata pesa za kufadhili miradi ya maendeleo, lazima raia watozwe ushuru lakini lazima ushuru uwe nafuu.

Haufai kutishia mpango wa kuzalisha nafasi za kazi nchini au kukandamiza umma. Rais Ruto amesahau mama mboga, bodaboda na watu wa vioski ndio walikuwa wakishabikia hoja zake na walimwezesha kuingia ikulu wakitarajia kupunguziwa gharama ya maisha.

Pendekezo la serikali katika Mswada wa Fedha 2023 kuwatoza walala hoi ushuru zaidi ni ishara tosha Ruto hajui kwa nini alivutia raia kumchagua Rais au ameamua kuwasaliti kwa kukubali mapendekezo ya ushuru mpya yanayoumiza raia.

Pendekezo la kupandisha ushuru wa kutuma pesa kwa njia ya simu kutoka asilimia 12 hadi 15 ni sawa na kushangilia Wakenya kuendelea kuishi katika mazingira magumu zaidi maana huenda wahisani wakaogopa kuwapa msaada wakitumia mfumo wa M-Pesa kwa kuogopa kutozwa ushuru.

Ruto ajue mahasla hawawezi kuendelea kuvumilia serikali inapoendelea kuwatesa na kuwa tishio katika maisha yao kwa kushindwa kutekeleza ahadi na matarajio ya mahasla wanaokufa kutokana na ukosefu wa usalama, ukosefu wa matibabu bora na watoto wao kukosa Elimu kutokana na ukosefu wa karo na sasa matumaini yao yameuliwa na pendekezo la ushuru mpya. Ikiwa Mkenya aliyeajiriwa atatozwa ushuru wa nyumba kutoka kwa mshahara wake mdogo watarajia maisha yawe nafuu lini?

  • Tags

You can share this post!

Gavana aunga kampeni ya ‘mtu mmoja, shilingi moja’

Huduma za M-Pesa kuzinduliwa nchini Ethiopia

T L