• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 3:09 PM
STEVE ITELA: Wahifadhi mazingira wakataa marekebisho ya Sheria ya uhifadhi wa misitu

STEVE ITELA: Wahifadhi mazingira wakataa marekebisho ya Sheria ya uhifadhi wa misitu

Na STEVE ITELA

SISI kama mashirika ya uhifadhi wa mazingira, tunapinga na kukataa mswada wa marekebisho ya Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Misitu (Mswada wa Sheria ya Bunge Na. 53 wa 2021).

Katibu mkuu wizara ya Mazingira na Misitu ameanzisha shughuli ya kuhakiki mswada wa kuhifadhi na kusimamia misitu ili iambatane na katiba ya 2010.

Tuna wasiwasi kuwa mabadiliko haya yanayolenga kutowahusisha wataalamu katika mapendekezo ya Huduma za Misitu (KFS) kwa Bunge la Kitaifa kuhusiana na kubadilisha au kuchukua ardhi ya misitu, yatadhoofisha ulinzi na usimamizi wa mashamba ya misitu ya umma.

Kihistoria, Kenya ilipoteza zaidi ya hekta 420 milioni za misitu kwa sababu ya ukataji wa misitu na matumizi mengine kabla ya mabadiliko ya sheria ya uhifadhi na usimamizi wa misitu 2016 ulioongeza ukuaji wa misitu (Sehemu ya 34).

Marekebisho haya yana mapendeleo na ubinafsi, ambayo yataathiri pakubwa usimamizi wa misitu ya umma.

Waziri wa Mazingira na Misitu, Bw Keriako Tobiko ameandika barua kwa bunge ili likatae na kutupilia mbali marekebisho hayo. Hii, ni ishara tosha kuwa mswada huo hauna manufaa kwa Wakenya.

Mashirika ya uhifadhi wa mazingira yanapaswa kuhusisha wizara husika, KFS na Tume ya Ardhi (KLC) kusuluhisha shida za misitu iliyoingiliwa na kuratibiwa na sheria.

Bunge la Kitaifa linashauriwa kusimamisha marekebisho hayo na kukubali wizari ya Mazingira, Kawi na KFS kuendelea na kazi nzuri ya kulinda misitu.

KFS inaombwa ikague ardhi na ekari ya misitu na kutoa mapendekezo kuhusu misitu iliyoingiliwa na kuwakilisha ripoti kwa bunge la kitaifa.

Wizara ya Mazingira na Misitu pamoja, KFS na serikali za kaunti zianzishe mikakati ya kuzuia uvamizi wa misitu ya umma.

Tunaliomba bunge la kitaifa limwache Bw Tobiko, aendekee kuipitia sheria hiyo uhifadhi wa misitu.

Bw Itela ni Afisa Mkuu Mtendaji, Conservation Alliance of Kenya

  • Tags

You can share this post!

Chelsea kukosa tegemeo Mount, Hudson-Odoi na Chilwell dhidi...

Raia waingiwa na hofu polisi wakiendelea kujiua

T L