• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
TAHARIRI: Azimio waunge upinzani thabiti kutetea raia

TAHARIRI: Azimio waunge upinzani thabiti kutetea raia

NA MHARIRI

BAADA ya Rais William Ruto kutangazwa mshindi wa urais na baadaye kuapishwa, viongozi na wafuasi wa muungano wa Kenya Kwanza wamekuwa wakisherehekea huku wapinzani wao wakisononeka.

Ni jambo la busara Wakenya kuelewa kwamba nchi hii ni yao na wanapaswa kuilinda kwa njia yoyote ile hata wakiwa katika hali gani.

Hivyo, walioshindwa hasa Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, wanafaa kukubali hali yao na kusonga mbele na maisha.

Kwa sasa hivi, viongozi hao ambao upande wao ulishindwa wanafaa kuungana pamoja kama kitu kimoja ili kuunga upinzani dhabiti na kutetea haki za Wakenya ambao wanawahitaji mno endapo serikali iliyoingia mamlakani itawadhulumu ama itakosa kuwafanyia wafaayo.

Inafadhaisha sana madai ya kulaumiana yakidaiwa kutokea muungano wa Azimio ambapo baadhi ya viongozi wanaelekezea kidole cha lawama Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohamed na gavana wa zamani wa Mombasa Ali Hassan Joho kushindwa kwa Raila Odinga kunyakua Urais.

Viongozi kama Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino wanafaa kukoma tabia hii na kupigania maridhiano ili kufanya kazi kama muungano dhabiti.

Ni jambo la kutia moyo kwa Rais William Ruto kusisitiza hilo Jumamosi alipotangaza kwamba serikali yake haitateua yeyote kuwa waziri ili kuzezesha kundi hilo kuwa na uwezo wa kukosoa endapo uongozi wake utaenda kombo.

You can share this post!

Kenya Kwanza ni piga ua kwa Azimio

Kipchoge alenga rekodi Berlin Marathon

T L