• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:55 AM
Kipchoge alenga rekodi Berlin Marathon

Kipchoge alenga rekodi Berlin Marathon

NA GEOFFREY ANENE

BINGWA wa Berlin Marathon mwaka 2015, 2017 na 2018 Eliud Kipchoge anaamini anaweza kuimarisha rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 42 ya saa 2:01:39 anayoshikilia atakapotimka mjini Berlin, Ujerumani mnamo Septemba 25.

Katika mahojiano na timu yake ya NN Running Team kuhusu historia yake ya Berlin Marathon, Kipchoge, 37, alisema, “Nimekuwa nikijiwekea malengo na kuyashughulikia kwa kuyamanikia. Tulisherehekea miaka minne iliyopita nilipokata utepe ndani ya rekodi ya dunia. Naamini bado ninaweza kuweka rekodi mpya mjini Berlin.”

Rekodi ya dunia ya 2:01:39 pia ni rekodi ya Berlin Marathon.

Muethiopia Kenenisa Bekele, ambaye wako timu moja na Kipchoge, alikosa rekodi hiyo kwa sekunde mbili akinyakua taji la Berlin Marathon 2019.

Atakayeshinda Berlin Marathon 2022 atapokea tuzo ya mshindi ya Sh4.7 milioni na kuongezwa Sh5.9 milioni akiweka rekodi mpya ya dunia. Baadhi ya wapinzani wa supastaa Kipchoge ni bingwa mtetezi Guye Adola kutoka Ethiopia.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Azimio waunge upinzani thabiti kutetea raia

Hit Squad ya Kenya yamaliza nambari 12 mashindano ya Afrika

T L