• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 6:17 PM
TAHARIRI: CBC: Machogu avae viatu vya Magoha

TAHARIRI: CBC: Machogu avae viatu vya Magoha

NA MHARIRI

RAIS William Ruto amemteua Ezekiel Machogu kuwa waziri mpya wa elimu, akisubiri kupigwa msasa na wabunge.

Mtangulizi wake Waziri Magoha atakumbukwa zaidi kwa mipango ya dharura ya kubadilisha ratiba za masomo tangu ugonjwa wa Covid-19 uingie nchini.

Aidha, atakumbukwa kwa kutetea mtaala mpya wa elimu wa CBC ambao unawakosesha baadhi ya watu usingizi.

Ni wazi kuwa kuna kibarua kigumu kilicho mbele ya waziri anayeingia Bw Ezekiel Machogu. Waziri Machogu atakabiliwa na mzigo wa kuhakikisha amefaulisha wanafunzi wa darasa la nane na wale wa gredi ya sita kujiunga na shule za sekondari.

Madarasa haya mawili yanatarajiwa kuingia kwa pamoja katika shule za upili hapo Januari 2023.

Wanafunzi hawa wapatao milioni mbili na nusu wanatarajia kupata nafasi katika shule chache za sekondari zilizoko nchini.

Licha ya waziri anayeondoka ,Prof Magoha kudhihirishia Wakenya kuwa madarasa mapya ya kuwapokea wanafunzi wa gredi ya 7 yamejengwa, wananchi wangali na shaka jinsi mambo yatakavyokuwa.

Aidha, waziri anatarajiwa kukabiliana ‘kiume’ na matatizo chungu nzima yanayotinga sekta hii ya elimu.

Ukosefu wa walimu wa kutosha shuleni ni tatizo ambalo linamsubiri. Shule nyingi nchini zina idadi ndogo sana ya walimu isiyoweza kukidhi mahitaji ya elimu bora kwa Wakenya.

Isitoshe, hata asilimia kubwa ya walimu waliopo hawajapata mafunzo ya kutatua shida za masomo nchini hasa katika masomo ya vyuo vya ufundi na mtaala mpya wa CBC.

You can share this post!

WALIOBOBEA: Karume: Mhimili, rafiki wa dhati wa Mwai Kibaki

JUNGU KUU: Ruto atakavyopanga ‘wazee’ Uhuru, Raila

T L