• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
TAHARIRI: Maonevu dhidi ya timu za Kenya zikicheza ugenini yakomeshwe

TAHARIRI: Maonevu dhidi ya timu za Kenya zikicheza ugenini yakomeshwe

NA MHARIRI

KATIKA mashindano ya Africa Zone 3 yaliyoandaliwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) mwaka jana 2021, timu ya taifa ya ndondi ilirudi nyumbani na jumla ya medali 12 kama ifuatavyo; dhahabu 1, fedha 5 na shaba 6.

Maafisa walioandamana na kikosi cha Kenya kipindi hicho waliamini mabondia wa Kenya walionesha mchezo wa hali ya juu na walistahili kushinda medali nyingi za dhahabu.

Kulingana na msemaji wa Shirikisho la Ndondi Nchini (BFK) Duncun Kuria, kiini cha upungufu wa medali hizi ni maamuzi yasiyofaa kutoka kwa wenyeji DRC.

Mnamo Novemba 2021, baada ya klabu ya soka Gor Mahia kushindwa , viongozi wake walilalamikia matukio ya uchawi pamoja na usimamzi wa timu ya AS Otoho d’Oyo ya Congo Brazzaville uliodaiwa kutumia ‘singizio’ la corona kuwafungia wachezaji wao bora nje ya mechi hizo za Kombe la Mashirikisho kati ya timu hizo.

Kati ya wachezaji tegemeo wa Gor ambao walikuwa wamezuiliwa kucheza mechi ya mkondo wa kwanza wakidaiwa kuwa na corona ni washambuliaji Benson Omalla na Samuel Onyango, kiungo John Macharia na beki Philemon Otieno.

Kinaya ni kwamba katika mechi ya mkondo wa pili, iliyosakatwa siku tatu baadaye, vipimo vilionyesha kuwa wachezaji hao hawakuwa wakiugua virusi hivyo hatari.

Kando na hilo, Gor walidai kuonewa na kabla ya mechi hiyo, kanda ya video iliyosambazwa ilionyesha afisa mmoja wa AS Otoho d’Oyo akiweka vitu fulani uwanjani vilivyoshukiwa kuwa vya uchawi.

Katika mashindano ya ndondi mwaka huu yanayoendelea nchini DRC, Kenya iliamua kuwakilishwa na jumla ya mabondia 22 ambapo bondia Christine Ongare na Gisele Nyembo wa DRC walipigana.

Ongare alishindwa na mpinzani wake katika raundi zote tatu.Lakini kwa mshangao Gisele (wa DRC) alipewa ushindi uamuzi uliopingwa vikali na maafisa wa Kenya waliokata rufani kulalamikia uamuzi huo usiofaa.

Maafisa wa Kenya walitisha kutoendelea na mashindano hayo hadi pale suala hilo litakapochunguzwa.

Baadaye waandalizi walibadilisha maamuzi hayo na kumpatia Ongare ushindi Jumatatu baada ya kubaini bondia huyo kweli alistahili ushindi.

Serikali, wasimamizi wa michezo wabuni mbinu za kuzuia na kukabili matui haya ambayo yanavunjwa moyo ya wanaspotiwetu wenye vipawa na uwezo usio kifani.

You can share this post!

DRC yajiunga rasmi na EAC

PSG kumpa Mbappe ofa mpya ya Sh23.4 bilioni ili asihamie...

T L