• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Ahadi ya mabwawa Nanyuki imekuwa ni ndoto isiyotimia

TUSIJE TUKASAHAU: Ahadi ya mabwawa Nanyuki imekuwa ni ndoto isiyotimia

MNAMO Jumamosi wiki jana, Naibu Rais William Ruto aliahidi kwamba serikali yake itajenga bwawa kubwa mjini Nanyuki akishinda urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Alidai kuwa mipango ya Serikali ya Jubilee ya kujenga mabwawa 57 makubwa nchini ilisambaratishwa na handisheki kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga mnamo Machi 9, 2018.

Safu hii inawakumbusha wakazi wa Nanyuki, ambao Dkt Ruto aliwapa ahadi hii, kwamba ahadi sawa na hiyo ilitolewa na serikali ya Jubilee mnamo 2013 ilipoanza muhula wake wa kwanza mamlakani.

Lakini haikutimizwa ndani ya miaka mitano ya utawala wa Jubileee wakati ambapo Dkt Ruto hudai kuwa alikuwa “Naibu Rais mwenye mamlaka makuu.”

Isitoshe, manifesto ya kwanza ya Jubilee iliyozinduliwa na Rais Kenyatta na Dkt Ruto kuelekea uchaguzi mkuu wa Machi 4, 2013 pia inasheheni ahadi hiyo hiyo ya ujenzi wa mabwawa.

  • Tags

You can share this post!

‘Mawaziri wako huru kuunga Raila mkono’

NJENJE: Ushuru mpya wa mayai watishia uhusiano wa...

T L