• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:05 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Akiwa Waziri Mkuu Raila alishindwa kutatua mzozo wa Migingo

TUSIJE TUKASAHAU: Akiwa Waziri Mkuu Raila alishindwa kutatua mzozo wa Migingo

MNAMO Alhamisi wiki jana, mgombea urais wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga aliahidi kuwa atatimua wanajeshi wa Uganda kutoka kisiwa cha Migingo akishinda urais Agosti 9.

Alitoa ahadi hiyo alipokuwa akiendesha kampeni za kusaka kura za urais katika eneo bunge la Nyatike, kaunti ya Migori.

Lakini Bw Odinga asije akasahau kuwa mzozo kati ya Kenya na Uganda ulianza mnamo 2009, maafisa wa usalama wa Uganda walipowanasa Wakenya wakiendesha uvuvi karibu na kisiwa hicho.

Wakati huo, kiongozi huyo wa ODM alishikilia wadhifa wa Waziri Mkuu katika Serikali ya Muungano Mkuu chini ya uongozi wa Hayati Rais Mwai Kibaki.

Afisi ya Bw Odinga, ambayo ilishirikisha majukumu ya wizara zote za serikali, ilishindwa kutanzua mzozo kuhusu umiliki wa kisiwa cha Migingo chenye utajiri mkubwa wa samaki.

Hii ni licha ya kwamba ramani ya utawala wa kikoloni inaonyesha kuwa kisiwa hicho kiko mita 600 ndani ya Kenya.

Licha ya serikali ya sasa kukariri kila mara kwamba Migingo ni mali ya Kenya, walinda usalama wa Uganda ameendelea kuwakamata na kuwatesa Wakenya katika kisiwa hicho.

  • Tags

You can share this post!

Shule za kibinafsi sasa tayari kwa CBC ya sekondari

Wezi wavamia kanisa na kuiba mali yenye thamani ya Sh250,000

T L