• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 10:48 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Munya asije akasahau Kiunjuri aliwezesha NCPB kupewa ruzuku ya Sh6 bilioni

TUSIJE TUKASAHAU: Munya asije akasahau Kiunjuri aliwezesha NCPB kupewa ruzuku ya Sh6 bilioni

BEI ya unga wa mahindi imeanza kupanda na kufikia hata zaidi ya Sh120 kwa pakiti ya kilo mbili kwa sababu kampuni za kusaga unga zimekabiliwa na uhaba wa mahindi.

Hali hii inachangiwa na hatua ya wakulima wa mahindi kudinda kuuza mahindi yao kwa Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB), wakitaka bei ya Sh3,500 kwa gunia la kilo 90.

Bodi hiyo inanunua zao hilo kwa Sh3,000 uzani huo huo.

Lakini Waziri wa Kilimo, Bw Peter Munya, anafaa kufahamu kwamba anaweza kuwakinga Wakenya kutokana na ongezeko la bei ya unga.

Bw Munya asije akasahau kwamba mnamo 2018, mtangulizi wake, Bw Mwangi Kiunjuri, aliwezesha NCPB kupewa ruzuku ya Sh6 bilioni kutoka kwa Hazina ya Kitaifa na kuiwezesha kupunguza bei ya mahindi kwa kampuni za kusaga unga wa mahindi.

Hatua hiyo ilichangia kushuka kwa bei ya unga kutoka Sh150 hadi Sh75 kwa pakiti ya kilo mbili.

  • Tags

You can share this post!

Kibicho aendeleza siasa, akanusha kutumia mabavu dhidi ya...

TAHARIRI: Serikali iseme ukweli kuhusu kuvuja mtihani...

T L