• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 7:52 PM
TUSIJE TUKASAHAU: NHIF ifanyiwe mageuzi iwahudumie Wakenya wote bila kujali magonjwa wanayougua

TUSIJE TUKASAHAU: NHIF ifanyiwe mageuzi iwahudumie Wakenya wote bila kujali magonjwa wanayougua

MAPEMA mwezi huu Shirikisho la Mashirika ya Kutetea Maslahi ya Wagonjwa wa Saratani (KNCO) lililalamika kuwa Bima ya Kitaifa ya Afya (NHIF) imedinda kugharimia matibabu ya wagonjwa wa saratani.

Viongozi wa mashirika hayo waliiomba Wizara ya Afya kuingilia kati suala hilo ili NHIF iwe ikilipia gharama yote ya matibabu haswa kwa wagonjwa ambao huchanga Sh500 kila mwezi kwa bima hiyo.

Lakini ikumbukwe kuwa mnamo Juni 29, 2017 Rais mstaafu Uhuru Kenyatta aliahidi kwamba katika muhula wake wa pili, NHIF ingelipia matibabu ya magonjwa kama vile saratani, kisukari na maradhi ya moyo.

Aidha, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, Rais William Ruto aliahidi kufanikisha mipango na miradi yote bora iliyoanzishwa wakati wa utawala wa Bw Kenyatta.

Isitoshe, katika manifesto ya muungano wa Kenya Kwanza iliyozinduliwa na Juni 30, 2022 Dkt Ruto aliahidi kuwa katika utawala wake, NHIF ingefanyiwa mageuzi ili iweze kuwahudumia Wakenya wote, pasi na kujali magonjwa wanayougua.

Vile vile, Rais Wiliam Ruto aliahidi kuwa kila Mkenya angesajiliwa kwa bima ya NHIF kufikia Desemba 2022. Bado tunasubiri!

  • Tags

You can share this post!

Kampuni yazindua simu inayolenga wasanii

Kura: Mungatana amtaka Kioni akome kudharau IEBC, mahakama

T L